Waziriwa Kilimo Profesa Adolf Mkenda anapataa wasaa wa kuzungumza na waandishi wetu, Jesse Kwayu, Absalom Kibanda na Neville Meena juu ya mipango na matarajio ya wizara hiyo katika kuleta mageuzi makubwa ya kilimo nchini. Miongoni mwa mambo yanayolengwa na serikali ni kuongeza uzalishaji kwa eneo. Yapo mengi amezungumza. Indelea kusoma…
SWALI: Wizara ya Kilimo imebeba sekta muhimu katika uchumi wa nchi. Usalama wa chakula kwa taifa unategemea kilimo, malighafi za viwanda vingi nchini zinategemea sana kilimo pia. Ni zipi juhudi, sera za wizara yako katika kusimamia dhima hii?
“Juhudi kubwa tunayoifanya sasa ni kuongeza tija kwa sababu tumeona kinachotatiza maendeleo ya kilimo na muunganiko wa kilimo na sekta nyingine ni tija ndogo.”
PROF. MKENDA:
Ni kweli Wizara ya Kilimo imebeba jukumu kubwa kwanza tu ajira,
tunachukua karibia theluthi mbili ya nguvu kazi inategemea kilimo moja kwa moja. Na vilevile usalama wa chakula, uhakika wa chakula tunategemea kwenye kilimo karibia asilimia 100, ukiondoa tu mifugo ambapo kwa kweli maana pana ya kilimo hua ni mazao, mifugo, uvuvi na misitu.
Lakini Wizara yetu sasa hivi ipo zaidi kwenye mazao kwa sababu maeneo mengine yako sehemu nyingine. Serikali inajaribu kuelimisha uzalishaji zaidi kwa ajili ya kuhakikisha kwanza tuna uhakika wa chakula nchini, na bahati nzuri tunajitosheleza chakula kwa ujumla wake. Lakini vilevile, tunajaribu kuhimiza na kuweka mikakati ya kuongeza tija kwenye kilimo. Na tija maana yake nini? Tija maana yake unapata kiasi gani kwa juhudi zote unazoingiza kwenye kilimo na tafsiri hiyo Kingereza inaitwa productivity.
Unapata kiasi gani kwa juhudi zote unazoingiza kwenye kilimo, maana yake ardhi uliyoingiza kwenye kilimo, nguvu kazi uliyoingiza kwenye kilimo, pembejeo unayoingiza kwenye kilimo na kadharika. Lakini tija wakati mwingine na mara nyingi zaidi tunazungumzia unapata kiasi gani kwa eneo unalolima hii Kingereza inaitwa yield kwa maana hiyo tija ina maana mbili moja ni productivity ambapo juhudi zote zinaingizwa katika uzalishaji na nyingine ni ardhi tu kwamba ekari moja unazalisha kiasi gani.
Kwa hiyo juhudi kubwa tunayoifanya sasa ni kuongeza tija kwa sababu tumeona kinachotatiza maendeleo ya kilimo na muunganiko wa kilimo na sekta nyingine ni tija ndogo. Na nitatoa mfano, kwenye pamba sasa hivi na tuna mikoa 17 inalima, lakini ukiangalia tunapata kilogramu 200 hadi 350 kwa ekari moja. Lakini ukiangalia kuna nchi hapo Afrika Magharibi wanapata kilo 1,000 kwa ekari.
nguvu kazi ya theluthi mbili inachangia theluthi moja tu kwa hiyo huwezi kushangaa kuna maeneo unapita unaona umaskini kwa macho, vijijini unaona nyumba zao wanazoishi.
Na kule Misri naambiwa kuwa wanafikia mpaka kilogramu 2,000, sasa ukisema unataka kwanza kuongeza viwanda vya kutengeneza nguo kwa sababu unalima pamba, lakini pamba yako uzalishaji wake ukawa na tija ndogo kiasi hicho kuna chanagmoto kubwa sana kwa sababu tunataka uwe mshindani. Na ile nguo utakayoitengeneza itakuwa na gharama kubwa kiasi kwamba ya kutoka nje itakuwa na bei ndogo zaidi na vile vile huwezi kuuza nje kwa sababu wenyewe watakuwa wanachukua pamba katika sehemu ambayo tija ni kubwa.
Mfano, katika mafuta ya kula sasa hivi sisi tunaagiza mafuta ya kula kutoka nje tunajitosheleza kwa takribani asilimia 45 tu ya mahitaji ya mafuta ya kula. Ukweli ardhi yetu inatosha kuzalisha mazao ambayo yanatoa mafuta ya kula ya kutosha tena na ya ziada kutoka nje ya nchi, lakini hatufanyi hivyo.
Mafuta tunayoagiza mengi ni mawese yanatoka Malaysia. Sasa kuna watu wanasema machikichi asili yake ni Kigoma na mawese yanatokana na michikichi, sisi tunaweza kulima michikichi na kupata mawese ya kutosha. Kinachokwamisha ni tija ndogo. Mpaka hapa tulipo tunazalisha kwa hekta moja ya michikichi tunapata tani 1.6 ya mafuta ya mawese kwa hapa Tanzania.
Tunaambiwa wenzetu kwa hekta moja wanapata mpaka tani 5, tena wengine wanasema mpaka tani 10. Sasa katika mazingira kama hayo ni vigumu sana kuondoka kuongeza ushindani, yaani kwenda kuacha kununua mafuta kule na kuanza kutumia mafuta ya ndani.
Naweza nikataja mfano wa zao moja hadi jingine, kwahiyo mkakati wetu mkubwa umelenga kuongeza tija hasa sasa hivi, na tija itatufanya tuwe washindani.
Namna ya kupima tija: Ukichukua nguvu kazi ya nchi theluthi mbili inatumika kwenye kilimo, theluthi moja ndo inafanya shughuli nyingine, lakini ukiangalia mchango wa kilimo kwenye pato la taifa ni asilimia 26 tu. Na hiyo asilimia ni kilimo kwa mapana yake, maana yake kilimo, mifugo, uvuvi, pamoja na misitu. Kwa sababu ukiangalia mazao tu mchango wa kilimo ni chini ya asilimia 20. Maana yake ni kuna mambo matatu muhimu:
Inaonyesha kwamba umaskini lazima utakuwa mkubwa kwenye kilimo kwasababu kile tunachokula nchini, tunachozalisha watu wote walioko kwenye kilimo wanachangaia kiasi kidogo sana, yaani nguvu kazi ya theluthi mbili inachangia theluthi moja tu kwa hiyo huwezi kushangaa kuna maeneo unapita unaona umaskini kwa macho, vijijini unaona nyumba zao wanazoishi.
Maana ya pili, ni kwamba uwiano wa mapato ni mbaya sana kwa sababu tunaposema theluthi mbili ya nguvu kazi inachangia theluthi moja tu ya pato la taifa na pato la taifa ndo ambalo ni kama keki maana yake unasema theluthi mbili ya watu wanakula theluthi moja tu ya keki.
Tatu, tija ni ndogo sana kwa sababu ukichukua mchango wote wa kiuchumi wa sekta zote unakuta ile iliyo na watu wengi inatoa mchango mdogo sana, kwa hiyo tija yake inakuwa ndogo.
Kwa hiyo hii muunganiko wa tija unaweza ukaungalia kwa ujumla wake kwa maana hiyo. Sasa unaweza ukaangalia kwa zao moja moja, ukichukua pamba, ukichukua mikorosho, michikichi na kila zao hata mihogo. Sisi mihogo tunapata kwa hekta moja
tunazalisha tani 3 hadi tani 8. Sasa hivi bahati nzuri utafiti umegundua tunaweza kuzalisha hadi tani 22, naambiwa mpaka tani 50 kidogo inanitia shaka, lakini wananiambia wataalamu.
Madhara yake tusipokuwa na tija nzuri, soko la China linahitaji mihogo hivyo tutashindwa kuuza. Lakini pia muhogo sio chakula tu ni chanzo cha wanga. Na nchi yetu tunaagiza wanga asilimia 100 kutoka nje ya nchi, wakati tunaweza kulima mihogo. Ukanda wote wa pwani unaweza kulima mihogo, lazima ujiulize kulikoni maana yake ni kwamba tija ni ndogo. Hatuna cha kutosha tule na kutengeneza wanga. Yako mengine, lakini sasa hivi tija ndo tumeibeba zaidi
Mikakati;
Kwanza; Utafiti kwa kuongeza bajeti ya utafiti kwa asilimia 53. Bajeti ya Wizara yetu haijaongezeka ndo ambayo tulikuwa nayo mwaka jana na juzi, ambayo ni bilioni 294. Hivyo tumejaribu kuangalia maeneo ambayo tutaokoa ili tuongezee huku. Na utafiti utakuwa ni kwenda kupata mbegu bora na kutambua kilimo bora. Na mfano wa matokeo ya utafiti tuliyokuwa nayo ni kwenye pamba. Kupitia utafiti wa namna ya kulima pamba, tumegundua namna ya kufanya nafasi (spacing) ya mche na mche na kuweka samadi au mbolea fulani inachanganywa pale Mijingu. Tunaweza na tumefanya majaribio tumeona kwa ekari tunaweza kupata kilo 1,000 hadi 1,400. Kwa hiyo utafiti ni muhimu, sasa hivi tunafanya kampeni kubwa katika mikoa yote ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija.
Kwa hiyo kipaumbele chetu cha pili ni kuhakikisha tunazalisha mbegu za kutosha.
Cha pili; Uzalishaji wa mbegu bora hapa nchini. Tuna uhaba mkubwa sana wa mbegu bora. Sasa hivi tunafanya kampeni ya alizeti na tumegundua hatuna mbegu za kutosha. Tuna mbegu yetu tuliifanyia utafiti inaitwa rekodi inazalisha vizuri, lakini kidogo mno wala haitoshi, haitatupeleka popote. Kwa hiyo wakati tunajaribu kufanyia utafiti kwenye mbolea yetu ya rekodi, lazima tuagize mbolea kutoka nje ya nchi.
Kwa hiyo kipaumbele chetu cha pili ni kuhakikisha tunazalisha mbegu za kutosha. Na tumeanza kampeni kwenye ngano inalimwa, lakini hatuna mbegu tunaagiza kutoka Zambia, viazi mbegu zinatoka Kenya. Kwa hiyo sisi tunchohitaji ni mbegu zetu kuzifanyia utafiti, zitakazohimili mazingira yetu tuweze kupata mazao ya kutosha. Na anayetakiwa kufanya utafiti huu ni wakala wetu wa mbegu anaitwa Seed Multiplication anayo mashamba 13, lakini mengine yameachwa kama mapori hivyo tunataka kuhakikisha mwaka huu mashamba hayo tunayafufua ili yaweze kufanyiwa umwagiliaji ili kuzalisha mbegu za kutosha.
Kwanza tumechagua mikoa mitatu ambayo ni Dodoma, Singida na Simiyu ambako tutafanya majaribio ya mfuno bora wa huduma za ugani (the prototype extension service) na tutafanya hivyo katika mikoa mingine. Lakini pia sasa hivi maofisa ugani wote tumewanunulia pikipiki.
Kipaumbele cha tatu ni huduma za ugani. Tumefanya mabadiliko makubwa sana kwenye wizara yetu, bajeti ya huduma ya ugani ilikuwa milioni 603 kwa mwaka. Sasa hivi tumeipeleka mpaka bilioni 11.3 na hazitoshi kabisa, lakini walau tumeweza kuokoa hela huku na kule na kuzipeleka kwenye huduma ya ugani. Na kwenye huduma ya ugani tumefanya mambo kadhaa. Kwanza tumechagua mikoa mitatu ambayo ni Dodoma, Singida na Simiyu ambako tutafanya majaribio ya mfuno bora wa huduma za ugani (the prototype extension service) na tutafanya hivyo katika mikoa mingine. Lakini pia sasa hivi maofisa ugani wote tumewanunulia pikipiki, na kwenye bajeti yetu tunapikipiki 1,500. Lakini bodi zetu zote za mazao tumeziagiza zifanye hivyo. Kwa hiyo bodi ya pamba maofisa ugani wote watanunuliwa pikipiki. Kwa sababu unakuta bwana shamba yuko kwenye kata hana hata baiskeli na anatarajiwa kila siku akiitwa aende.
Pili, tunafufua na kuendeleza mashamba darasa kila maeneo kwa kuhakikisha yanakuwepo, yanalimwa vizuri ili wakulima waone yanakuwa mfano kwa jinsi ambavyo wanaweza kuvuna kama wakiendesha kilimo bora.Tatu, Mabwana shamba hawa wote tunawasaidia walime wao mashamba yao, tutawasaidia na pembejeo walime vizuri. Na tunafanya hivyo kwa sababu mbili, kwanza ili ilikujua kama anafanya kazi yake vizuri na pia waweze kupata mapato. Tunanunua vifaa vya kupima afya ya udongo ambavyo vitakuwa kwenye halmashauri na hawa watafundishwa namna ya kuzitumia. Kuna sehemu ukipewa mbolea ya namna fulani inabidi kwanza uchanagnye na chokaa, sehemu nyingine unaweza ukaitumia bila kuchanganya, lakini ili ujue hayo ni mpaka uwe na hiki kifaa. Na pia tunawanunulia maofisa ugani simu ambapo kuna kuwa na App wanajaza kila siku kueleza alichokifanya. Na tunaamini katika hii mikoa mitatu tukifanya vizuri tutakuja kuongeza kutokana na bajeti ya serikali