26.4 C
Dar es Salaam
HomeKilimo BiasharaMaswa yajipanga kuongeza uzalishaji zao la pamba

Maswa yajipanga kuongeza uzalishaji zao la pamba

Na Samwel Mwanga, Maswa

HALMASHAURI ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imejipanga kuongeza uzalishaji wa zao la pamba kwa msimu wa mwaka 2023/2024 kwa kulima hekta 60,438 kwa uzalishaji wa wastani wa kilo 400 kwa ekari moja lengo likiwa ni kuwainua wananchi kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Robert Urassa wakati akitoa taarifa fupi ya utekekezaji wa zao la pamba wilayani humo, wakati wa mafunzo ya kilimo bora cha zao hilo kwa madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Maswa.

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu wakiwa kwenye mafunzo ya kilimo Bora cha zao la pamba yaliyotolewa na Bodi ya Pamba Tanzania(TCB)

Amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na kuhakikisha wanasimamia upatikanaji na ugawaji wa pembejeo za pamba ambazo ni mbegu, viuatilifu na vinyunyizi vinapatikana kwa wakati kwa kutosheleza mahitaji ya wakulima wa zao hilo wilayani humo.

Ameendelea kueleza kuwa wamepanga kutoa elimu ya kilimo bora cha zao hilo kupitia mashamba darasa hivyo kila afisa ugani wa kata atapewa malengo ya kuanzisha shamba darasa moja la zao la pamba katika kila kitongoji.

“Tumepanga kutoa elimu ya kilimo bora cha zao la pamba kupitia mashamba darasa hivyo kila afisa ugani wa kata atatakiwa kuanzisha shamba darasa moja la zao la pamba katika kila kitongoji,”amesema.

Pia amesema watarikisha viongozi wa Serikali na wale wa kisiasa kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji, kata hadi wilaya katika uhamasishaji na usimamizi wa zao hilo sambamba na kuwahamasisha wakulima wenye mbolea ya samadi wanapekeka shambani mapema kwa kutumia utaratibu ulioelekezwa.

Balozi wa pamba nchini,Agrey Mwanri(aliyenyoosha)mkono akisisitiza jambo kwenye mafunzo ya kilimo Bora cha zao la pamba kwa madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Maswa.

Naye Balozi wa pamba nchini, Agrey Mwanri amesema kitendo cha halmashauri hiyo kukubali madiwani hao kupatiwa mafunzo hayo ni mojawapo ya utekekezaji wa Agizo la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan la kutaka Mkoa wa Simiyu kuzalisha tani 500,000 za pamba hadi kufika mwaka 2025 huku wilaya ya Maswa ikipewa lengo la tani 130,000.

“Mlichokifanya halmashauri ya wilaya ya Maswa ni jambo la Msingi sana kutoa elimu ya kilimo bora cha zao la pamba kwa madiwani ili muweze kufikia malengo ambayo mmewekewa ya kufikia tani 130,000 ya zao la pamba ifikapo mwaka 2025 sisi bodi ya pamba tutaendelea kuwaunga mkono kwa kuendelea kutoa elimu ya kilimo bora cha zao la pamba ili wakulima wazalishe kwa tija,”amesema Mwanri.

Aidha, amewataka madiwani hao kushirikiana na viongozi wengine wa serikali kuhakikisha wakulima wanalima kilimo cha pamba kwa kufuata kanun zake kwenye maeneo yao na wale wanaokwenda kinyume washughulikiwe kwa mujibu wa sheria zilizowekwa za zao hilo.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Maisha Mtipa amesema kuwa mafunzo hayo yana lengo ya kuwajengea uwezo madiwani hao wa halmashauri hiyo juu ya kilimo bora cha zao la pamba ili wawe sehemu ya wasimamizi wa kilimo hicho tangu kuandaa shamba hadi kuuza sokoni zao hilo kwenye maeneo yao.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Maswa, Athuman Kalaghe (aliyesimama) akifungua mafunzo ya kilimo bora cha zao la pamba kwa madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Maswa.

Aidha, amesema kuwa zao la pamba ndicho chanzo kikuu cha mapato ya ndani katika halmashauri hiyo hivyo ni lazima waweke nguvu kubwa katika Kilimo hicho na kuhakikisha zao hilo linalimwa kwa kufuata kanuni zote za kilimo bora cha zao la pamba ili kuhakikisha mkulima mmoja mmoja anazalisha kwa tija.

Pia ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuhakikisha zao la pamba linazalishwa kwa tija kwa serikali kuendelea kuwajali wakulima kwa kuwapatia pembejeo kwa mkopo.

spot_img

latest articles

explore more

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here