27.2 C
Dar es Salaam
HomeMwelekeoTanzania kuwa kitovu cha chakula Afrika

Tanzania kuwa kitovu cha chakula Afrika

Na Mwandishi Wetu, FAMA

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amesema Serikali imeweka mikakati itakayotekeleza nchi kuwa kitovu cha chakula Afrika na duniani kote ili iweze kunufaika na tishio la njaa linalo ikabili dunia.

Mikakati hiyo ni pamoja ile ya kibajeti, kisera, teknolojia, kiuwekezaji na ushirikiano baina yake na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

Hayo yanatokea wakati takwimu zinaonyesha wananchi barani Afrika watakaokabiliwa na upungufu wa chakula wataongezeka na kusababisha kiasi cha fedha za kigeni zitakazotumika kuagiza chakula kuongeza.

Dk. Mpango amebainisha hayo Septemba 5, jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Jukwaa la Mfumo ya Chakula Afrika (AGRF) unaojumuisha watu 5,000 kutoka nchi 70 za Afrika.

Amesema mikakati ya kibajeti ni pamoja na kuongeza bajeti kwenye sekta ya kilimo kutoka Dola milioni 120 kwa mwaka 2021/2022 hadi kufikia dola milioni 397 kwa mwaka 2023/2024 iliotolewa na Serikali ili kuboresha sekta ya kilimo.

“Tunawashkuru AGRF kwa kuandaa mkutano huu, kwa kushirikiana na Serikali naamini unakwenda kuleta matokeo chanya,huku akisisitiza mada zitakazojadiliwa zilenge kwenye uzalishaji wa chakula haijalishi tuko na hali gani,” amesema Dk Mpango.

Amesema hiyo inaonyesha jinsi gani Serikali imejikita kuwekeza katika kilimo hasa ukizingatia sekta ya kilimo inamgusa kila mmoja.

Amesema hii ni bahati kubwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu kwa mara ya pili naonyesha jinsi gani ilivyojipanga kuhakikisha sekta ya kilimo inapiga hatua kwenye kilimo ili kuwainua wananchi wake kiuchumi.

Amesema ili kuhakikisha sekta ya kilimo inakua kwa kiasi kikubwa ni lazima ishirikishe vijana na wanawake na kwamba ndio sababu kuna programu ya vijana ya BBT ambayo imejumuisha vijana waliojikita katika kilimo cha aina mbalimbali.

Amesema ili kuhamasisha vijana kuingia katika kilimo Serikali imeanzisha kilimo cha umwagiliaji chini ya programu ya Jenga kesho iliobora (BBT) ambayo iliwajumuisha vijana wakike na wakiume ambao wamehitimu mafunzo na kukabidhiwa maeneo kwa ajili ya kuendeleza kilimo mbalimbali.

Amesema ili kuhamasisha vijana kuingia katika kilimo, Serikali imeanzisha kilimo cha umwagiliaji chini ya programu ya Jenga kesho iliyobora (BBT) ambayo iliwajumuisha vijana wakike na wakiume ambao wamehitimu mafunzo na kukabidhiwa maeneo kwa ajili ya kuendeleza kilimo mbalimbali.

“Katika mikakati ya kisera, Serikali inathamini mifumo ya chakula,mipango ya mabadiliko ndio maana imejitolea kushirikiana na AGRF na hii ni kutokana na kutambua malengo muhimu ya sDG-2 ili kufikia asilimia sifuri kwenye baa la njaa ifikapo 2030,” amesema Dk. Mpango.

Aidha, amesema Serikali imewekeza pia katika uwepo wa ghala ya chakula kwenye Kanda, Taifa na Kimataifa, hii ni kutaka kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo.

Akizungumzia mikakati ya kiteknolojia Dk. Mpango amesema ni pamoja na kupanga mikakati ya ufuatiliaji sekta ya kilimo kupitia teknolojia ya kisasa kama kutumia vishkwambi ndege zisizo na rubani kwa ajili ya kuangalia kuna changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, zinazowakabili wakulima.

Ameelezea kuwa kutokana na hali hiyo Serikali imeongeza uwekezaji katika utafiti, ili kuongeza uzalishaji wa mbegu bora ambazo zitachangia kuzalisha chakula kwa wingi kitendo ambacho kitachangia kupunguza fedha ambazo hutumika kuagiza chakula nje ya nchi.

Naye Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Afrika ina ardhi ndogo huku ikikadiriwa ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na ongezeko kubwa la watu, hivyo wanapaswa kuwekeza katika suala zima la kilimo chenye tija.

Upande wake Waziri wa Uvuvi na Uchumi wa Blue wa Zanzibar, Suleiman Masoud Makame amesema kuna haja ya kuungana dhidi ya madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya tabaia nchi, kwa kuongeza uzalishaji na kukuza ujuzi wa mifumo ya chakula.

spot_img

latest articles

explore more

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here