27.2 C
Dar es Salaam
HomeMahojianoMaajabu ya nyuki: Mdudu mdogo anayezalisha mazao manane ..(ii-1)

Maajabu ya nyuki: Mdudu mdogo anayezalisha mazao manane ..(ii-1)

SWALI: Kuna mfano wowote ambao katika kupitapita kwako umeshuhudia tiba za aina hii zikitolewa au kufanyika kwa ufanisi?

 

JIBU: Ndiyo. Mimi nimesoma pia mambo ya nyuki pia Korea ya Kusini. Huko Korea ya Kusini karibu kila wilaya kuna Apitherapy Centre, Uturuki kuna Apitherapy Centre, ukienda New Zealand kuna Apitherapy Centre, Apitherapy Centre ziko China, hizi ni muhimu sana. Kwa hiyo afya za watu, yaani mimi binafsi nikiumwa nina uwezo wa kujitibu nyumbani hata kama ni malaria.

Kwa sababu kwa mfano dawa ya malaria inatengezwa na nini? na miti, ambayo nyuki ndiye anakwenda kuichukua hiyo miti na ameitengeneza na ninapokula pollen ina maana ni mchanganyiko wa hiyo miti kwa pamoja, hivyo kuufanya mwili wangu kuongeza chembehai nyekundu za damu. Na rahisi tu, ukumwona mtu ana udhaifu maana yake selihai nyekundu za damu zimepungua. Na zimepungua kwa sababu zimeliwa na plasmodium au zimeliwa na wadudu wa viumbe wa magonjwa mengine.

“Lakini pia kuna watu wana mtindio wa ubongo, kuna watu wanakuwa creasy – creasy kidogo, akili hazifanyi kazi; hawa watu ukiwatengenezea program.”

Kwa hiyo maana yeke leo mimi naweza kumpa pollen, nikamg’atisha nyuki na baada ya muda yule mtu akapona akawa vizuri. Maana kinachoangaliwa ni kile kinachokwenda kuua ile plasmodium. Kwa hiyo utafiti unaweza kuendelea kufanyika kwenye mazingira yetu, lakini kwa maana ya nje mimi sina shida kabisa watu wanatibiwa. Lakini pia kuna watu wana mtindio wa ubongo, kuna watu wanakuwa creasy – creasy kidogo, akili hazifanyi kazi; hawa watu ukiwatengenezea program ya kuwang’atisha nyuki wawili kila siku hapa (anaonyesha kwenye mashavu) wawili kwa mara moja ukiwa umewashika katika mikono yote miwili; maana yake mtu wa aina hiyo unamshtua, kwa hiyo unakuwa ume-trigger vitu fulani kuamka kwenye mwili.

Ukifanya program hiyo kwa mwezi au kwa miezi miwili mtu anapona. Mimi naona kuna fursa kubwa. Ninachosema ni kwamba dawa zinazoagizwa kutoka nchi za nje, mimi nilikwenda Misri kwenye viwanda vya kutengeneza dawa mwaka 2016/2017 wakaniagiza malighafi za kutengeneza dawa na mojawapo ilikuwa ni simu ya nyuki. Sasa kumbe zile dawa sisi tunaziagiza kutoka kule, na zinaweza kutengenezwa kwa sumu ambayo sisi tunayo huku na sisi tunaweza kupata hiyo sumu ikiwa fresh. Kwa hiyo kwa maana nyingine ni kwamba hapa tuna uwezo na kila kitu. Kupitia misitu tunaweza kufanya mambo mengi.

sasa kwa nini sasa hivi tumekimbilia iodine tincture tumeacha hii ya asili, kwani asali imewahi kufeli popote?

Vijana wanaosoma ufamasia (pharmacy), wanaosoma vyuo vikuu, wanaosoma biashara, nawaomba wasizione ofisi kama vile ziko Kivukoni Front. Wasizione ofisi kuwa ziko Makao Makuu ya Dodoma. Waone ofisi ziko msituni. Wakiona msitu wauite ofisi na waingie wafanye kazi. Tutagundua vitu vingi ambavyo vitasaidia jamii yetu. Mfano nikianzisha apitherapy ni kawaida maana hata wazazi wetu na mababu zetu walikuwa wakitibu kwa kutumia asali.

Ulikuwa ukikohoa kidogo unapewa asali, ukiumwa hiki unapewa asali, ukiungua moto unapakwa asali, sasa kwa nini sasa hivi tumekimbilia iodine tincture tumeacha hii ya asili, kwani asali imewahi kufeli popote? Tuwaulize waliotumia asali labda, iliwahi kufeli? Haijawahi kufeli. Kwa hiyo mimi naona kwamba wazo letu hili la kuanzisha apitherapy center litapokelewa vizuri na Watanzania na pia nchi nyingine jirani.

Hivi ni vitu ambavyo watu wenyewe tunaweza kufungua haraka kwa sababu malighafi yanapatikana katika maeneo yao. Kuliko kuagiza dawa iko kwenye meli miezi minne au haifiki mapema, mimi naona tutapunguza gharama, tena gharama ya serikali ya Tanzania kuagiza madawa mengi kutoka nje na ile burden kupungua. Pia kwa njia hiyo tutaongeza ajira na hivyo vitu ambavyo tunavijua ni vizuri zaidi kuvitumia.

SWALI: Mbali utaalamu wa kumng’atisha mtu nyuki, huu ukusanyaji wa sumu ya nyuki unafanyikaje?

 

JIBU:

Kwanza kabisa uvunaji wa sumu ni rahisi kuliko zao lolote, halafu ni muda wote. Yani sumu inavyunwa muda wote, japokuwa muda mzuri zaidi wa kuivuna ni usiku. Wataalamu wa sumu wanatuambia kwamba usiku ndipo nyuki wanahifadhi sumu nyingi kwa sababu hawaoni. Kwa hiyo wanajiandaa kukabiliana na chochote kinachoweza kutokea. Kiasilia wanakuwa na sumu nyingi kwenye ile bladder (kimfuko cha sumu ambacho kinahifadhi sumu).

Sasa ile sumu inatolewa kwa njia ya sting ambayo iko sehemu ya nyuma ya nyuki. na aking’ata mara nyingi utaona kama anaacha ule mwiba ambao unatakiwa uutoe. Sasa aking’ata huwa ni kama lile bomba la sindano ya kuchoma watu. Ile syringe imetengenezwa kwa mfano wake kutoka kwenye nyuki, maana ikishakuchoma bado huwa kuna kazi ya kusukuma, ndo maana mtu aking’atwa na nyuki unaambia kuondoa ile sting haraka.

Sasa kwa nyuki unamtengenezea kaka kioo kwa chini pamoja na wavu, akiwa na hasira anakuja kung’ata kwenye kile kioo na sumu inabaki hapohapo kwenye kioo.

Sasa kuna mashine zinaitwa bee venom collector ambazo tayari Watanzania wameanza kuzitengeneza na hata sisi tulikuwa tunashirikiana na Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kujaribu kutengeneza hiyo mashine ya sumu ya nyuki. Hiyo mashine inatengeneza vibration (mtetemo) ambayo ni ndogo sana na zile vibration zinawakasirisha sana nyuki. Ni kama wewe mtu akuletee bati hapa halfu awe analipiga wakati wewe ukiwa umepumzika kwa hiyo utaamka haraka na utataka kushughulika naye. Sasa kwa nyuki unamtengenezea kaka kioo kwa chini pamoja na wavu, akiwa na hasira anakuja kung’ata kwenye kile kioo na sumu inabaki hapohapo kwenye kioo.

Baadaye ukija kukwangua hicho kioo, unaipata sumu ikiwa kwenye hali ya unga na siyo kwenye kimiminika. Ikiwa hivyo basi hiyo ndo sumu tayari ambayo ni ghafi. Na hiyo sumu ukiweza kupata gramu moja bei yake yaani market outlook duniani ni kama dola 200 sawa na laki nne au laki tano kwa gramu moja. Na ukiweza kupata kilo moja ya sumu ni zaidi ya Sh. milioni 280. Na hii nisije nikawafanya wafanyakazi walioajiriwa waache kazi zao, kwa sababu unaweza kupanga programu ya kutafuta sumu ya nyuki kilo moja ndani ya miaka miwili ukapata milioni zaidi ya 200 na kitu.

Sisi vijana wa sasa hivi ukituambia utuajiri kwa kweli tunaona kama tutapita mapito yale yale ya baba zetu ambayo ni magumu.

Ukifafanisha na kusubiri kiinua mgongo kwa miaka 30 au kwa miaka 30 ya utendaji wa kazi kunakuwa na tofauti kubwa. Sisi vijana wa sasa hivi ukituambia utuajiri kwa kweli tunaona kama tutapita mapito yale yale ya baba zetu ambayo ni magumu. Kwa hiyo sisi tunawashauri wazee wetu waendelee kufanya kazi kama kawaida, ila sisi tutaangalia mechanism nyingine za kujisimamia wenyewe kwa kutumia hizi rasilimali ambazo ni kubwa zaidi.

Mimi nimependa sana hapa Singida na hakuna sehemu ambayo naipenda kama hii ya Kijiji cha Nyuki. Napapenda sana maana hata kama nikisafiri kwenda nchi za nje, huwa natamani kurejea haraka. Kuna siku nilishuka Dar es Salaam kwa ndege saa moja asubuhi kutoka Canada, nikawahi gari pale Ubungo zamani ili niweze kuwahi kuja Singida. Yani hata kutua tu pale Dar es Salaam naona kama nitakuwa napoteza muda. Lakini nikikaa huku, nikiona misitu, nikiona maji, nikiona asali na nikiona mazao nafurahi sana. Nikila vitu vya asili huku, kama mlivyoona nakula miwa yaani ni safi kabisa.

spot_img

latest articles

explore more

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here