27.2 C
Dar es Salaam
HomeMahojianoPinda atoboa ya moyoni hisia zake kwa kilimo (ii)

Pinda atoboa ya moyoni hisia zake kwa kilimo (ii)

SWALI: Mheshimiwa Pinda umezungumza vizuri kuhusu Kilimo Kwanza. Lakini unazungumzia vipi kuhusu changamoto za pembejeo, masoko na mambo kama hayo? Je, unafikiri kilimo hiki cha Kitanzania kinaweza kweli kuwa mkombozi wa kuinua watu kama ulivyosema au kinaonekana kama ni shughuli ya kujikimu tu watu wapate chakula au hata kama kuna ziada ni kuuza kidogo tu? Hili unaweza kulizungumzia je?

JIBU: Tuseme ukweli tu, kama tulivyosema kuwa ukishakubali kuwa asilimia 70 ya watu wako vijijini na tegemeo letu ni kilimo, tegemeo letu ndani yake jambo la kwanza ni usalama wa chakula.  Wasipokuwa na chakula cha kutosheleza kulisha familia utaingia kwenye mgogoro mkubwa sana. Kilimo hicho tunasema ni cha kujikimu. Ni cha kutufanya tule na kushiba, lakini kama hujaenda hatua moja mbele na kukifanya ni cha kibiashara ili  alime, apate chakula, apate ziada ili aweze kuleta cha ziada ambacho. Ndiyo wengine sasa wanatarajia hata kulima anaweza kuyapata hayo ya ziada.

“Tuseme ukweli tu, kama tulivyosema kuwa ukishakubali kuwa asilimia 70 ya watu wako vijijini na tegemeo letu ni kilimo… jambo la kwanza ni usalama wa chakula.”

Sasa kwa historia ya nchi yetu tangu tumeanza ni kwamba tunalima kilimo cha namna gani. Kilimo chetu ni cha jembe la mkono, sasa tuliona safari ya jembe la mkono inakuwa ndefu sana ndiyo maana nyakati tofauti yalikuja mawazo ya jinsi ya tutakavyoweza kutumia kulima vizuri zaidi na kwa haraka zaidi. Sasa hapa ndipo ulipoanza kuona maarifa yanaingizwa kama mechanization, matumizi ya zana za kisasa za kilimo. Matumizi ya zana yalitakiwa kuzingatia mazingira halisi ya Kitanzania wapi tulipo.

Mwanzoni kabisa tulikuwa tunazungumzia matumizi ya majembe ya kukokotwa na ng’ombe au wanyama. Lile ni rahisi kuweza kumfundisha mtu, lakini yataleta mabadiliko. Hayawezi kufafana na pale alipokuwa analima kwa jembe la mkono. Hapana. Kutakuwa kuna tofauti kwa huyo mtu. Lakini wakati ule tulipokuja na wazo hili la Kilimo Kwanza, katika kuongeza nguvu ya zana za kilimo, ndiyo tukaingia katika matumizi ya matrekta. Lakini bado baada ya kuangalia hali ya vijijini tukasema tuje na haya matrekta madogo. Tuakaja na dhana ya power tillers. Baadaye tukapanda ngazi hadi matreta madogo, lakini pole pole tukaja na wazo la kuweza kutumia matrekta makubwa.

wakati ule tulipokuja na wazo hili la Kilimo Kwanza, katika kuongeza nguvu ya zana za kilimo, ndiyo tukaingia katika matumizi ya matrekta.

Lakini yatolewe katika mfumo ambao utawezesha eneo kubwa, kijiji labda, au kikundi kikubwa cha wakulima wapate nafasi ya kulitumia lile trekta vizuri zaidi. Maana huwezi kuwa na trekta halafu unalima heka 10. Hapana, hiyo siyo uchumi hata kidogo. Lakini hili lilisaidia sana maana watu waliona kumbe trekta linaweza kulima heka nyingi. Ikageuka ikawa ni kama biashara kwa watu wengine. Unaagiza trekta na ukawa unakwenda kulima kwenye mashamba ya watu wengine. Kwa hiyo hizi jitihada mbalimbali za serikali kusema kwa kweli zimesaidia kwa kiwango kikubwa sana na fikra mpya kwa wakulima, ndiyo maana mwanko huo mpya ukaja sasa sambamba na mawazo ya mbegu bora ili uweze kuongeza tija katika zao lolote ulilokuwa unalitumia. Lakini vile vile tukazungumza habari ya mbolea kwa maana kilimo peke yake bila mbolea unaweza uzalisha, lakini siyo kwa kiwango kile ulichotarajia. Kwa hiyo, maarifa haya yote, mbinu hizo zote zikaanza kuingizwa katika kilimo na ndiyo kwa kweli kilianza kuleta faraja kwa wakulima wengi. Na tulifaulu sana.

Tulipoanza kupeleka haya mawazo mapya wakulima wengi walibadilika vizuri sana, na maeneo mengi wakaanza kujenga vijumba vizuri zaidi, nyumba za bati tofali za kuchoma tena kama sisi Rukwa na uchawi ukaisha kabisa. Maana wakati ule ukijenga nyumba bora kila mtu anakodolea macho. Wanasema haiwezekani, maana wanakuambia wewe ukijenga shauri yako kwa maana watakuloga tu. Lakini sasa utamloga nani, kwa maana kila mtu ameshaamka na ana uwezo. Kwa hiyo kuna vitu vingi vizuri vimetokea pale, lakini bado nadhani kwa maoni yangu nguvu hiyo hatujafika mahali tukasema itelekezwe  kwa sababu wameshakubali kila kitu kiko sawa.

Ndiyo maana bado naona kwa mfano, ukiangalia kilimo eneo la soko sasa hivi limegeuka kuwa ni tatizo kubwa. Tunalima kweli mahindi, lakini ni nani mnunuzi? Unalima mpunga, nani mnunuzi? Nimelima pamba, nani ananunua? Sasa hili si jambo dogo, ukitaka kweli kumsaidia mkulima kuweza kukamilika, ni lazima suala la soko lipewe nafasi kubwa sana. Ndiyo maana wakati ule serikali ya awamu ya nne Rais aliamua wakati ule kwamba NRFA (Wakala wa Taifa wa Nafaka) ambaye alikuwa na kazi tu ya kununua chakula kwa ajili ya akiba, anunue chakula kutoka kwa wakulima hawa, aweke katika maghala yao. Kwa maana ana uwezo hata wa kuuzia majirani zetu. Ila kwanza mkulima awe na uhakika kuwa ana soko. Ndiyo maana tukafaulu mahindi yale tukayapandisha kufika kilo moja Sh. 500. Kwa hiyo, akiuza gunia moja la kilo 100 ana Sh. 50,000. Na wakati ule ilikuwa ndiyo kilele hasa, sasa tungetamani kutoka hapo twende Sh. 600, Sh. 700. Kwa sababu walaji wa ugali tupo na ni wengi na si Tanzania tu mpaka nchi jirani. Kwa hiyo, nadhani pamoja na jitihada zilizofanyika kwa kiasi cha kutosha, lakini nadhani tumekwenda vizuri.

Upande wa pili ni lazima pia tukubali kwamba hizi taasisi za utafiti kwenye kilimo, pamoja na vyuo vikuu vyote vimesaidia sana katika kusogeza sekta ya kilimo kupata uelewa mpana na wa haraka. Ndiyo maana leo ukiona tukirudi nyuma katika jambo fulani kelele zinaongezeka, safari hii hatukuletewa hiki, safari hii mmechelewa kuleta hiki kwa sababu ule mwamko ule umesukumwa pia na taasisi za kitafiti ambazo zilikuwa zinatafiti juu ya mbegu bora, ni mbolea gani itumike, ukifanya hiki, ukijaribu kutumia hiki unaona kweli mambo yanakuja kwenda vizuri. Kwa hiyo, nisema hiyo imeendelea, lakini nasema bado tunahitaji kuongeza kasi kwa sababu tunataka kuona nafasi ya umasikini huku chini ikitoweka.

ni lazima suala la soko lipewe nafasi kubwa sana. Ndiyo maana wakati ule serikali ya awamu ya nne Rais aliamua wakati ule kwamba NRFA (Wakala wa Taifa wa Nafaka) ambaye alikuwa na kazi tu ya kununua chakula kwa ajili ya akiba, anunue chakula kutoka kwa wakulima hawa, aweke katika maghala yao.

SWALI: Tanzania tunapakana na nchi takriban kumi, zikiwa ni zile za Afrika Mashariki na SADC. Ni ipi changamoto ambayo inatukwaza kiasi cha kushindwa kuingiza mazao yetu hasa ya chagula katika masoko ya nchi hizi?

JIBU: Ni kweli Tanzania tuna bahati tumezingirwa na nchi karibia nane tisa zinatuzunguka na kwa sehemu kubwa. Ni kweli kujua demand ipo, lakini si kwamba kuhisi ndio nchi pekee, kuna nchi nyingine vilevile zinazalisha chakula na kwa namna moja au nyingine kuna kuwa na taratibu za kubadirishana mazao hayo na fedha au na vitu vingine.

Lakini kama unavyosema nadhani kiwango ambacho pengine tunatumia fursa hiyo, pengine si kikubwa sana. Panahitajika nguvu ya ziada, vilevile kuona masoko haya yanayotokana na nchi jirani namna bora ya kuweza kuhakikisha yanatumika vizuri. Maana moja kubwa unaloliona pale ni sheria zetu wakati mwingine na taratibu zetu juu ya mazao kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.

ni eneo ambalo kiukweli liko bado dhahiri kwetu kwamba ni fursa ambayo tukijipanga vizuri, tukastadi vizuri jinsi gani wangependa na nini, bado tuna nafasi kubwa tu.

Kwa hiyo lazima pawepo hali kidogo ambayo inarahisisha watu kuweza kuruhusu kupeleka vyakula mahali pengine, ilimradi tu zile taratibu zisiwe kali wakati mwingine unnecessarily katika mazingira ambayo pengine haikuwa lazima sana, ingawa wakati mwingine nchi inalazimika vilevile kulinda soko lake la ndani. Kwa hiyo wakati mwingine akiweza kuzingitia ni kwa sababu wakulima nchini kwake wamezalisha kiasi cha kutosha na asingependa tena mazao mengine yakaingia mahali pale ambayo yanaweza yakapatikana kwa bei nafuu. Kwa hiyo anaona hapana ngoja nilinde soko la ndani, watawakatalia tu. Lakini bado kama unavyosema ni eneo ambalo kiukweli liko bado dhahiri kwetu kwamba ni fursa ambayo tukijipanga vizuri, tukastadi vizuri jinsi gani wangependa na nini, bado tuna nafasi kubwa tu.

SWALI: Mh. Pinda wewe ni kiongozi na hapa tumeona changamoto ya pembejeo na masoko, urahisi kidogo ambao umeupata mpaka ukaweza kuwa na eneo hili la hekari 70 na ukaendelea kuzimudu na kuzifanyia kazi, unaizungumziaje nafasi yako ya uongozi katika kuwezesha urahisi huo, ikilinganishwa labda na mtu ambaye hajawahi kupata nafasi ambayo umeipata? Maana wapo wanaodhani kwamba kwa nafasi yako imekuwa rahisi kufika hapa ulipo leo.

spot_img

latest articles

explore more

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here