SWALI: Mh. Pinda wewe ni kiongozi na hapa tumeona changamoto ya pembejeo na masoko, urahisi kidogo ambao umeupata mpaka ukaweza kuwa na eneo hili la hekari 70 na ukaendelea kuzimudu na kuzifanyia kazi, unaizungumziaje nafasi yako ya uongozi katika kuwezesha urahisi huo, ikilinganishwa labda na mtu ambaye hajawahi kupata nafasi ambayo umeipata? Maana wapo wanaodhani kwamba kwa nafasi yako imekuwa rahisi kufika hapa ulipo leo.
JIBU: No hawakosei wanachosema ni kweli kabisa, kina ukweli ndani yake, ila upande mwingine ni jambo ambalo naona nalo vilevile wanalisema ni kuona kama maajabu, kuona Waziri Mkuu, huyu jamaa ambaye alikuwa kiongozi kwa miaka karibu saba nane anakuja anaendelea na kilimo si akae tu. Kwani hapati posho ya kumtosha kweli ya kuweza kuishi na familia yake, kwa hiyo wapo wanaowaza hilo alafu baadaey wanageuza, lakini mbona yeye analima kwa nini na mimi nisilime, sitalima kama yeye, lakini angalau naweza na mimi nikasukuma jambo, kwa hiyo nadhani ni pande zote mbili.
“unapokwenda bungeni kwa mara ya kwanza unakuta mabenki yote yanakuja kuwaona na kila mmoja anajaribu kukwambia kwamba mimi ndio bora kuliko benki nyingine.”
Sasa kurejea kwenye swali lenyewe la msingi, ukiwa kiongozi nataka kutumia mifano halisi hapa, ukiwa kiongozi na hasa nianzie nilipokuwa nimepata nafasi nikiwa bungeni lakini na huku ni waziri, baadaye nikaja kuwa waziri mkuu, moja ya jambo ambalo niliona ni jepesi sana kuliko kama usingekuwa ni pale unapokwenda bungeni kwa mara ya kwanza unakuta mabenki yote yanakuja kuwaona na kila mmoja anajaribu kukwambia kwamba mimi ndio bora kuliko benki nyingine.
Ukikopa mimi nitafanya hivi na hivi, lakini unaona kumbe wamelenga kundi hili kwa sababu ya uhakika wa malipo yao. Wanakuja wanakubana kwenye posho yako, kopa lakini tutakata moja kwa moja kwenye posho. Inatoka huko ikiwa imeshakatwa kwa hiyo unaona alaaa kumbe kauongozi nako haka sio kabaya. Ni kazuri, tatizo linakuwa tu ni kwamba umekopa unakwenda kutumia kufanya nini, hilo moja.
Lakini ukiwa bungeni pale kingine ambacho nilikiona kwangu ilikuwa ni jambo zuri sana, umebanwa sana unataka kufanya jambo fulani sasa wakati mwingine benki unaona masharti makali kidogo, ilifika mahali tukaona kwa nini tusuwaruhusu wabunge, kwani kapensheni kako mpaka miaka mitano si kanajulikana utapapa kiasi gani? Kwa hiyo unaweza kukopo aganist your pension mradi isizidi asilimia fulani, kakawa ni kadirisha kengine. Sasa dirisha hili ukalitumbukize serikalini kwa watumishi wa serikali inaweza isiwee rahisi sana, lakini kwenye political world huku lilikuwa linawezekana. Lakini lile ilikuwa ni kwa nini, kwa sababu tu unajua ni miaka yako mitano utapata kapensheni kako kisha tunalipana pale.
Kwa hiyo unaweza kukopo aganist your pension mradi isizidi asilimia fulani, kakawa ni kadirisha kengine.
Kwa hiyo ni kweli kabisa unapokuwa kwenye nafasi ya uongozi kwa upande huo unaona hata kwenda benki kukopa, inakuwa ni rahisi maana wanauhakika kabisa security kubwa pale ni Salary Slip yako kuliko unapokuwa hauko katika nafasi za kiuongozi kwa maana ya siasa mradi ni kiongozi.
Ndio maana vijana wengi wanapokuja hapa wakiwa bado wanafanya kazi na nini, hata wale wanaokuja kuona watafanyaje kabla ya kuli retire moja ya jambo nalisema kwa nguvu sana kipindi rafiki cha kukopa ni wakati ambao bado upo serikalini. Ukitoka maswali yatakuwa mengi, hata kale ka dhamana kataibuka kwa nguvu sana kuliko ulipokuwa Serikalini.
Kwa hiyo kopa, lakini tumia vizuri. Lakini ukiangalia upande mwingine vilevile, ukiwa serikalini humu, wewe unapiga kelele unasema hujapata mbegu za kupandia, mimi sipigi kelele mi nitasema jamani naweza kupata kilo 40 za mbegu, heshima ile ambayo umeitengeneza kati yako na wao watakupatia hizo kilo 40 unawalipa unakwenda unapanda.
Sasa mtu mwingine inabidi upike kafoleni ungoje, kwa hiyo ni kweli kabisa ka uongozi kana advantage za namna hiyo kwa upande mmoja, kwa hiyo lazima ni kiri ka swali kako ka hovyo hovyo kidogo, lakini bado ni suala tu la je, ulichokipata umekitumia vizuri? Au umekitumia kwa mambo ambayo unakuta unasema lakini hapa nimekula hasara bure bora ningepanda hata miembe ingekuwa nafuu zaidi.
Na ndio maana kwenye kilimo kila wakati nawaambia usije ukaja hapa ukakuta miembe inatoa maua mazuri mno ukadhani ni kazi ya siku moja, hapana, hii miembe tumeanza kuipanda mwaka 2003 na ndio maana leo ukija unaikuta hipo hivyo. Ni kazi inayochukua ka muda kidogo, lakini ukiwa na mpango mzuri wa polepole polepole polepole tutafika tu.
SWALI: Unaweza kuwashawishi Watanzania kwa kilimo kinalipa? Kwa mfano hata bila pensheni unadhani kilimo kinaweza kukuweka vizuri katika maisha yako yote?
JIBU: Ningekuwa na mimi nina nafasi ya kukuuliza na mimi ningekuuliza wewe unafikiri ni jambo gani ambalo utalifanya ambalo unadhani litakupa mambo kwa haraka haraka hivi, unaona maana ukigeuza sana kwangu umenibana kwenye kilimo, kwa hiyo unataka kujua kwamba kwa kilimo wewe unaona kweli ndio mahali stahili?
SWALI: Yes maana kuna watu wamewekeza kwenye real estate wakatafuta maeneo wakajenga apartments anakusanya kodi na hana stress yoyote maana ikifika mwisho wa mwezi anawatafuta wapangaji kudai kodi.
JIBU: Unaweza ukafikiri watu hao wanaodai kodi hawana stress, mimi mara ya mwisho nilimtembelea mzee wa Sumry bus (marehemu) baada ya kuona kwamba ameachana na biashara ya mabasi, ameamua kwenda kulima, nikavutiwa sana ikabidi nimfuate shambani nikamwambia we mzee vipi, wewe ulikuwa unatamba na mabasi ya Sumry bus, Sumry bus sasa vipi tena unakuja huku? akacheka akasema tatizo mkituona hivi mnatuona matajiri wakubwa tuna raha sana, akasema sio kweli hata kidogo.
ikabidi nimfuate shambani nikamwambia we mzee vipi, wewe ulikuwa unatamba na mabasi ya Sumry bus, Sumry bus sasa vipi tena unakuja huku?
Alichofanya nikajifunza maana aliniambia kabisa kwamba shughuli hii unayoiona ya mabasi ni complex kwa maana kwamba, kwanza si rahisi kwa pesa zako mwenyewe ukaibuke na mabasi hayo, labda kama umeiba pesa sijui wapi, kwa hiyo lazima utakwenda benki, na benki utavutana pale mpaka uje ufahulu, watakuanza kidogo kidogo ebu nenda kwanza kafanye kwanza kiasi hiki.
Sasa unafanya hiyo biashara, lakini kila ukikaa unaangalia trip unazotengeneza, kile unachopata, unaangalia matengenezo ya gari, mishahara ya watu mwisho unaona hii biashara hii….Mwisho akaniambia unafika mahali unazoea kwa maana ya kwamba nipo barabarani, nitakwenda nitarudi, nitakwenda nitarudi nakaa najua hata nikipata kidogo siku hiyo si haba naridhika. Lakini ukianza kuwaza kwa undani kabisa, anasema hapana, kwanza mabasi yakiondoka matano yanakwenda safari za nje, ukisikia simu usiku moyo unadunda sijui limedondoka sijui limefana nini, nikamuelewa.
Lakini na mimi nikamuuliza swali hilo hilo, sasa na wewe uliona kweli mahali pa kwenda ni kilimo, akasema ndio niliona ni kilimo na si kuja huku kwa kurukia tu aahaaaa ilikuwa ni baada ya kuwa nimefanya
unajua unapokuwa unaamka unafanya jambo na unaliona matokeo yake, kwa hiyo anasema yeye pale akilala akiamka akikuta mashamba aliyolima, maharage yamestawi vizuri, mahindi yamependeza anasema haaaaa yaani unajisikia vizuri sana.
uchunguzi, mwisho nikaona hapana nadhani kwenye kilimo kuna nafuu, yeye alitumia neno nafuu, ndio kuna nafuu.
Na mwishowe akaniambia kwa hiyo nipo hapa, wakati nilipokwenda ndio alikuwa kama mwaka wake wa pili au wa tatu hivi, akasema sasa hivi nani napaka usingizi. Changamoto zipo, lakini haziwezi kufanana na zile zilikuwa zinanipa presha. Akaanza kunitajia baadhi ya changamoto, mbegu bora wakati mwingine kuzipata inakuwa shida na ukipata waswahili wajanja wengine wanakuingiza mkenge, lakini hizi amesema zinatibika kwa urahisi.
Lakini kubwa alilolisema, akasema unajua unapokuwa unaamka unafanya jambo na unaliona matokeo yake, kwa hiyo anasema yeye pale akilala akiamka akikuta mashamba aliyolima, maharage yamestawi vizuri, mahindi yamependeza anasema haaaaa yaani unajisikia vizuri sana.
Nikamwambia haaa kumbe tupo wengi na haka kaugonjwa. Sasa akaniambia mabasi yale likienda likirudi mwaka mzima badala ya kuona linakuletea faraja, unajikuta kila mwaka unazidi kuporomoka kwa sababu ya gharama za matengenezo na kadhalika.
Nikamwambia basi vizuri, kwa hiyo brother niseme tu, kilimo kwangu mimi kama nilivyosema ni uasili ndio ulionifanya mpaka nikatumbukia kwenye kilimo, na ndani ya uasili ule pamoja na akili za utotoni, lakini kulikuwa na wakati una find comfort katika kilimo unaona.
Sasa unapokuja kuwa mtu mzima unakaa unaamini hivyo hivyo kwamba nadhani bado nitapata ka faraja fulani kwenye kilimo. Sasa nilipokuja kuanza kilimo chenyewe, ndo unakwenda. Unafika mahali unaona kumbe na huku changamoto zipo, lakini ni changamoto ambazo ukiwa makini zinaweza zisikupate, ukiondoa tatizo la kukosa maji kwa sababu mvua hazikunyesha, nyingine zote ni zile ambazo una uwezo nazo na ndio maana, kitu kimoja mpaka leo nakiona nastahili kabisa na nakuwa specific zaidi ni ile tu kwamba pamoja na udogo wa eneo hili tumechanganya mazao hapa karibu aina mbalimbali mifugo, kidogo tunayo asali, samaki, embe zimepandwa safari hii.
Sasa ukivichanganya vyote vile, unafika mahali unaona sio mbaya, nadhani nimeangalia vigharama vyangu na haka nilikokapata, sikupata kikubwa sana lakini nimevuka pale ambapo nilikuwa nimetegemea. Sasa huyo ni mimi naliwaza, lakini ukienda vijijini atakwambia alicholima, alichopata na comfort aliyoipata, utaona kabisa bado kuna hilo vile vile, ukiondoa ile necessity kwamba lazima ule na necessity kwamba kama unataka mtoto wako asome ada itatoka shambani, kwa hiyo hana mbadala.