imeonekana kwamba ni anti-aging. Watu (binadamu) wanaweza wakala ili wasizeeke haraka. Sasa ambao hawapendi kuzeeka nchini nafikiri wako wengi sana. Kwa hiyo soko la hii product ni la moja kwa moja. Na mimi naiuza na ninawajua wateja wangu
SWAL: Hii Royal gel inapatikana vipi?
JIBU: Ukitaka kuvuna royal gel kuna namna ya kuivuna na inavunwa na watu wanaozalisha makundi ya nyuki. Kweye uuzaji wa malkia wa nyuki, siku ya saba anaweza akaamua ni kama wewe unavyoweza kuamua iwapo ule yai la kuku au usubiri lije kuwa kifaranga. Kwa hiyo ukiamua kusubiri lije kuwa kifaranga ndiyo hapo unauza malkia mkubwa, kama unauza malkia. Lakini ukiamua kula yai maana yake ndiyo hiyo royal gel inavunwa.
“Sasa unaweza ukashangaa kwamba pamoja na bei hiyo watu wanakula.”
Kwa hiyo siku ya saba ndiyo kale kayai ka malkia kanakuwa kamewekwa kwenye hilo sega. Na kwenye sega kuna milligram mbili mpaka tatu. Kwa namna hiyo ukikusanya miligramu 50 zinauzwa Sh. 250,000 na lita moja inauzwa Sh 5,000,000. Sasa unaweza ukashangaa kwamba pamoja na bei hiyo watu wanakula. Kama mimi huwa navuna na inaisha.
Watu wanakula, sijawahi kuona na ni tofauti na nilivyofikiri mimi kwamba watu hawajui soko, lakini kumbe watu wanajua na wamekuwa wakiifuata huko nchi za nje tena kwa gharama kubwa. Sasa wanaposikia inazalishwa kwenye nchi yao, wanahamasika zaidi na sisi tunapata kipato. Kwa hiyo mimi humu ndani nikizalisha hiyo gundi, nikazalisha hayo maziwa ya nyuki, pia kuna pollen au chavua ya nyuki, mapato ni mazuri. Chavua hii inapatikana pale nyuki anaporuka halafu kwenye miguu anakuwa amebeba vidude fulani.
Hao ndio wanapaswa wale hili vumbi la Singida. Simply ni kwamba hawa watu hawana lishe nzuri.
Akienda kwenye mzinga tunamwekea pale mtego ambao unasababisha adondoshe zile chavua, kumbe ule ndiyo mlo kamili wa nyuki wa kila siku. Kwa hiyo watu wa nutrition na watu wengine kama madaktari kumshauri mtu ale mlo kamili, na ili uweze kula mlo kamili kwa wakati mmoja ni ghali maana itabidi ununue papai, utanunua nini…nini…ili uweze kukamilisha mahitaji. Unaweza kununua vitu vya Sh. 300,000 sokoni ili upate huo mlo kamili, ni ghali kweli. Lakini kwenye hii bee pollen kuna vitu vyote ambavyo unavitaka.
Yaani vituo vyote unavyoweza kununua kwa hiyo 300,000 vinapatikana kwenye kijiko kimoja tu cha pollen au chavua au vumbi la Singida kama wanavyoita. Unapokula unakuwa na mgawanyo mzuri wa vyakula ndani ya mwili wako na una-activate enzyme kufanya kazi yako vizuri. Mfano kuna watu wameteseka hawapati watoto, kuna watu wameteseka miili tu imekuwa dhaifu hawana nguvu za kutosha, akitembea kidogo anapumzika tu. Hao ndio wanapaswa wale hili vumbi la Singida. Simply ni kwamba hawa watu hawana lishe nzuri.
Wanaweza kuwa wanakulwa nyama, wanakula ugali, wanakula kuku hivyo wanafikiri kuwa expensiveness ndiyo diet, hapana. Wataalamu wa lishe wanaendelea kushauri watu wale mlo kamili, lakini watapata wapi mlo kamili? Hawana hela za kutosha. Hii bee pollen inauzwa kilo moja Sh. 300,000 na ulaji wake ni kula gramu 10 (sawa na kijiko kidogo) kwa siku. Na watu wanaishabulia, toka niitangaze mwezi wa tatu mwaka huu nilitangaza rasmi na nilikuwa na magunia manne, lakini sasa zimebaki kilo 40 tu.
Tena wanaokula ni wale wanaofahamu huo mlo muda mrefu na wengine ni wale ambao pengine alionjeshwa na aliyenunua na baada ya kula akapata nguvu. Hao wamekuwa wakija kununua bila hata maswali mengi. Kwa hiyo mimi ninaona kama Watanzania tuna fursa ya kuwekeza zaidi kwenye uzalishaji wa hili vumbi la Singida kama ikiwezekana. Huko kwenye mizinga mimi naweza kuwafungia hivyo vifaa maana mimi hizo kilo 40 zilizobaki zinaweza kuisha mwisho wa mwezi huu (Agosti 2021). Kwa hiyo mwezi wa tisa (Septemba) kutakuwa hakuna kabisa bee pollen nchini Tanzania. Mwezi wa kumi (Oktoba) hakuna, hadi mwezi wa 11 (Novemba) ndipo nitavuna. Na mimi ndiye mvunaji pekee hapa Tanzania, sina roho mbaya nashauri ili tuwe wengi. Kwa hiyo naogopa kwenda hata kwenye chombo cha habari kutangaza, kwa sababu nikitangaza nina kilo 40 tu ndizo zimebaki.
Ukiumwa na nyuki kumbuka kuwa kuna wadudu wengine wenye sumu kama nyoka wengi ambao wengi wao pia hutengeneza antibodies za ku-fight dhidi ya sumu ya aina hiyo.
Ukitangaza inabidi uwe umehifadhi mzigo mkubwa godown au niwatangazie watu wavune au niandae mafunzo ili niwafundishe watu jinsi ya kuvuna, hapo sawa. Hiyo ni bee pollen, product nyingine ni sumu ya nyuki. Sumu ya nyuki unaweza kuivuna moja kwa moja (direct) au ukatengeneza vaccine (chanjo) kwa ajili ya watu kuingiziwa kwenye miili yao kwa njia ya sindano (injection). Ijapokuwa ukitamka injection watu wengine wanashtuka kidogo kwa sababu ya hali iliyopo sasa, lakini mimi nina mpango wa kutengeneza injection (sindano) za kuwachoma watu au wachomwe direct (moja kwa moja) na nyuki.
SWALI: Sumu ya nyuki inasaidia nini?
JIBU: Inauwezesha mwili ku-develop (kutengeneza) antibodies (kinga). Ukiuimwa na nyuki kumbuka kuwa kuna wadudu wengine wenye sumu kama nyoka wengi ambao wengi wao pia hutengeneza antibodies za ku-fight dhidi ya sumu ya aina hiyo. Hizi ni message (ujumbe) kwamba ukiona kitu kinakug’ata kwenye mwili na unauma ujue kwamba hiki siyo kitu cha kuingiza mwilini. Sasa mwili unapojaribu kujizuia (kupambana) na hiyo hali ni kama wewe ulikuwa na nyumba, lakini ikawa imechukuliwa na kimbunga, lazima tukukute ukiwa kwenye nyumba nyingine baada ya muda. Umepataje, umefanyaje ni wewe utajua mwenyewe.
Kwa hiyo tutamchanganyia pollen, ile royal gel, tutamchanganyia asali kidogo, mwezi mmoja tu mambo yanakaa sawa.
Ila sasa hii sumu ya nyuki programu itakayoanzishwa ni kwamba walau mtu ang’atwe na nyuki mara moja kwa mwezi. Unaufanya mwili wako uwe imara zaidi. Sisi Kijiji cha Nyuki Co.Ltd tuna mpango wa kuwekeza kwenye Kliniki za mazao ya nyuki. Yani mtu akiumwa, akisikia mwili wake ni dhaifu asichague kwenda hospitali, badala yake achague kwenda kwenye kliniki ya masuala ya nyuki. Kwa mfano mtu hana mtoto, sisi tunajua jinsi ya kumchaganyia mazao ya nyuki na kupata mtoto. Sasa kule hospitali, daktari nenda akakwambie calculation kwamba ni hormone imbalances na nini ila sisi tutakwambia hii ni hormone imbalance, lakini pia ni suala la lishe yako siyo nzuri. Kwa hiyo tutamchanganyia pollen, ile royal gel, tutamchanganyia asali kidogo, mwezi mmoja tu mambo yanakaa sawa.