Nilipata mafunzo kule ya kufuga nyuki kibiashara na niliporudi hapa sijawahi kutoka. Nimeanzisha hii shughuli ya Kijiji cha Nyuki na kutoka kwenye hii ekari moja ambayo baba alinipa, nikanunua tena hili eneo ambalo tuko hapa, nikanunua tena eneo jingine kwa jirani yetu, ekari nyingine, hapa nilipojenga kiwanga nilinunua tena kutoka kwa mtu mwingine, mpaka sasa nimenunua ekari 5,000 katika Kijiji hiki cha Nyuki.
Nimekuwa na umiliki wa namna mbili; kwanza ni urithi na katika namna nyingine ni kununua kwa njia ya mikataba na kila kitu. Sasa hivi nina mpango wa kusajili hili eneo kama Private Beekeeping Reserve. Nimeshirikiana na familia pamoja na majirani ili kuona ambavyo nyuki wanaweza kututoa kimasomaso. Lakini nikiri kwamba tangu nimeanza kufuga nyuki sijawahi kupata hasara.
“Tuseme; hakuna madawa, hakuna kuwapa chakula, hakuna kufungulia asubuhi wala kufungia jioni kama wanyama wengine.”
Hata ukiangalia ripoti zetu za ukaguzi zinaonyesha faida toka day one (mwanzo) mpaka leo kwa sababu kwenye ufugaji huu wa nyuki kuna uwekezaji mdogo na usimamizi mdogo. Tuseme; hakuna madawa, hakuna kuwapa chakula, hakuna kufungulia asubuhi wala kufungia jioni kama wanyama wengine. Hakuna kuwaangalizia malisho na ufugaji wa nyuki pia ukiweka mizinga leo inakaa miaka 40 mpaka 50 bado mizinga ipo. Mizinga ya babu yangu mimi miwili bado ipo mpaka leo. Mizinga ya baba bado ipo. Na mimi nimeongeza mizinga, mpaka leo ninayo 20,065.
Kwa mizinga hiyo 20,065 kama mlivyoona mzigo unavyoshuka kiwandani maana yake kwanza nina order kubwa na asali inaisha mapema na ninazalisha tani 465 za asali kwa mwaka. Lakini mimi naona kwenye asali ni kama hakuna fedha kubwa, fedha kubwa zaidi iko kwenye mazao mengine ya nyuki kama sumu ya nyuki, maziwa ya nyuki, vumbi la Singida (bee pollen) kwa sababu lile kilo moja ni Sh. 500,000. Kama mwaka huu nilivuna magunia manne na kwa sasa hivi zimebaki kilo kama 40 na zote zimeuzwa. Ukiangalia kwenye mapato ni zaidi ya milioni 180 za pollen tu.
Watu walisema mimi ni Freemasons, watu wakasema mimi ni mchawi, watu wakasema mambo mengi kwa sababu tu ya nyuki.
Sasa asali hata kama ni hizo tani 465 thamani yake inaweza isifikie hiyo ya pollen kwa kuuza. Mimi niliona kama hatua ya kuanzisha Kijiji cha Nyuki pia niliona partner wangu asiwe mtu mwingine ila awe baba yangu. Hii kampuni ni yangu kwa asilimia kadhaa na baba yangu. Na nimechukua model fulani ambayo itahakikisha kwamba pasiwe na kelelekele nyingi, bughudha nyingi maana unajua partners wakiwa hawahusiani kidamu, kuna shida inaweza ikatokea halafu biashara ikayumba.
Naona kama baba yangu amenirithisha hii sehemu hili eneo la asili ambalo liliachwa na babu. Babu yule wa kwanza kabisa aliyefika hapa kwenye hili eneo kama nilivyosema hili eneo ninalimiki kwa urithi na kwa kununua, alifika mwaka 1780 alikuwa ni babu yangu yule anaitwa Mufonga ndiye aliyefika hapa akitokea maeneo ya Kondoa.
Kiasili kabisa sisi ni Warangi ila kwa sababu sasa vimepita vizazi vingi ndiyo tunakuwa Wanyaturu, hakuna mtu aliyebaki ambaye anasimama kuwa asili. Nimefuatilia historia na hapa ndani kuna makumbusho mengi ya mambo ya nyuki, yanaonyesha kwamba babu zangu walijificha wakati wanatafutwa na Wamasai. Kundi la Wamasai lilikuja kuteka ng’ombe. Sasa kuna eneo pale panaitwa Ifonelo karibu na mto pale kuna jiwe liko pale, lile linafahamika kama mzinga wa watu wote hapa
Lakini pia tunapanga kujenga makumbusho hapa na pale (Iponelo) ndipo tunapanga kujenga makumbusho ya nyuki. Hivyo ndivyo nilivyoanza, mwanzoni nilikuwa kama najaribu jaribu, lakini baadaye nikazamia hukuhuku. Ila kuna siku niliwahi kuachana na nyuki, mwaka 2015 ule niliwahi kufikiria kuacha nyuki baada ya watu kuniita majina mengi. Watu walisema mimi ni Freemasons, watu wakasema mimi ni mchawi, watu wakasema mambo mengi kwa sababu tu ya nyuki. Nikajiuliza kwa nini nisemwe hivi? Lakini baadaye nikapiga moyo konde nikaamua kuendelea.
SWALI:Tulio wengi kwa uelewa wetu tunafahamu kwamba zao la nyuki ni asali, lakini kwa ulivyotwambia ni kwamba nyuki ana mazao mengi kwa maana kwamba ziko bidhaa nyingi zinazotokana na nyuki, unaweza kutufafanulia kuhusu bidhaa hizo?
Nyuki ana mazao takriban sita ambayo unaweza kuyaingiza yote sokoni kabisa tukiachilia ukweli kwamba hata nyuki mwenyewe anauzwa.
JIBU: Nyuki ana mazao takriban sita ambayo unaweza kuyaingiza yote sokoni kabisa tukiachilia ukweli kwamba hata nyuki mwenyewe anauzwa. Lakini kuna zao jingine linaitwa ‘supu’ya nyuki kwa hiyo ukiyaunganisha yote unaweza kupata mazao kama manane hivi. Ukiangali sijui kama kuna mnyama au mdudu yoyote ambaye bila kumuua unaweza kupata mazao zaidi ya matano. Kwa mfano kuku anatoa mayai bila kumuua, ng’ombe maziwa bila kumuua, lakini nyuki anaweza kutoa mazao matano bila kumuua.
Unaweza kuona kwamba kwa kufuga kitu kimoja unaweza kupata mazao hayo matano bila kumuua yeye, ukiamua na yeye kumuuza unapata faida kubwa zaidi. Sasa mazao ya nyuki, ukiacha asali kuna nta ambayo ni by-product baada ya kuchakata asali na nta inauzwa bei mara mbili ya bei ya asali kwa kilo, maana kama asali inauzwa Sh.10,000 basi nta inauzwa Sh.20,000 kwa kilo moja. Kwa hiyo unaona zao ambalo ni by-product ndiyo ghali zaidi ya zao halisi. Sijui kama kuna zao jingine kwenye wanyama na wadudu, ambako lile zao la kwanza ni bei ndogo halafu ile by-product yake ni bei kubwa.
Kile chakula ndicho ambacho kina nutrient (virutubisho) nyingi kuliko chakula kingine chochote kwenye mzinga, anatengenezewa tu malkia ili aweze kuishi muda mrefu.
Sasa kwenye nyuki tunauona huo utofauti. Lakini zao la pili ambalo ni nta inatumika kutengenezea sabuni, lotion na pia inatumika kufanya moulding ya haya matenki ya stainless-steel kwa ajili ya chakula. Nta pia inatoa zao jingine linaitwa gundi ya nyuki, hii ni product ambayo ndo strong antivirus, antibacterial na ant- fungus, yaani yenyewe hakuna bacteria, kirusi wala fungus anayeweza kukaa mle. Kwa maana nyingine ni kwamba ile inatumika kutengeneza madawa kama iodine tincture ambayo ukisaifishia kidonda kinageuka kuwa chekundu na kinapona.
Ni vitu ambavyo Watanzania wengi wanaweza kufundishwa wakaelewa kwa lugha rahisi wakiwa majumbani humo humo. Kuna zao linaitwa maziwa ya nyuki (kwa kiingereza linaitwa royal gel), royal gel ni chakula ambacho hula malkia (wa nyuki) peke yake kwenye mzinga. Kile chakula ndicho ambacho kina nutrient (virutubisho) nyingi kuliko chakula kingine chochote kwenye mzinga, anatengenezewa tu malkia ili aweze kuishi muda mrefu.
Nyuki wanaokula ile wanaishi miaka mitatu mpaka mitano wakati nyuki ambao hawali royal gel wanaishi siku 58 mpaka 60. Ile product baada ya kuchunguzwa vizuri maabara.