SWALI: Tangu mwanzo wa mahojiano haya umekuwa ukizungumzia Kijiji cha Nyuki, kwa maelezo mafupi unaweza kusema hiki Kijiji maana yake nini?
JIBU: Kijiji cha Nyuki ni aina ya ufugaji wa nyuki na siyo kwamba ni eneo. Hii ni aina ya ufugaji wa nyuki, kwa Kingereza tunasema it is a collection of bees keeping activities in a workplace. Kama hii unavyoiona hapo kuna mizinga na shughuli nyingine, kwamba kila kitu unachokitaka hapa kipo. Kwa hiyo wazo hili la Kijiji cha Nyuki nililianzisha mimi hapa ulimwenguni.
“Kwa hiyo kwa sasa hivi kitu kipya duniani ambacho kinafahamika kwamba ndiyo the way forward pale unapotaka kufuga nyuki vizuri, ni kuanzisha Kijiji cha Nyuki.”
Baadaye niliitwa Umoja wa Mataifa nikafanya wasilisho (presentation), ukiingia kwenye mtadao utaona bees’ village and cities, liko Jiji la Nyuki na Kijiji cha Nyuki. Lakini pia, federation ya wafugaji nyuki duniani na wenyewe walipokea hii concept. Kwa hiyo kwa sasa hivi kitu kipya duniani ambacho kinafahamika kwamba ndiyo the way forward pale unapotaka kufuga nyuki vizuri, ni kuanzisha Kijiji cha Nyuki. Watu wengi kutoka Afrika Kusini, Nigeria, Zimbabwe, Botswana na Rwanda, wamekuja hapa kujifunza njia hii ya kisasa ya ufugaji wa nyuki ambayo wameanza kuisambaza na kuitumia katika maeneo yao.
Kwa hiyo Kijiji cha Nyuki ni kwamba tu kimeanzia hapa, na hapa ndiyo hiki kinaitwa Kijiji cha Nyuki. Na mimi kampuni kuiita Kijiji cha Nyuki ni kuipa ile thamani ya wazo lilipoanzia hapa. Sasa hivi katika nchi ya Tanzania tutaanzisha vijiji vingi vya nyuki. Mfano katika mkoa wa Singida mimi nimepanga nisaidie kuanzishwa kwa vijiji 230. Dodoma nataka nianzishe vijiji 120, lakini nitakwenda kuanzisha vijiji pia katika mikoa ya Iringa na Morogoro.
baadaye watu hawataanzisha umoja wa wafugaji wa nyuki kama watu wanavyofikiri kama mtu mmoja mmoja.
Kule kwenye majarida ya ufugaji wa nyuki ya Afrika, utakiona Kijiji cha Nyuki kiko front, kikiwa kama mwanzo mzuri unaopewa nafasi zaidi katika ulimwengu wa nyuki. Na hii ni wazi kwamba hili wazo litakua sana, baadaye watu hawataanzisha umoja wa wafugaji wa nyuki kama watu wanavyofikiri kama mtu mmoja mmoja, bali sisi tutaanzisha Umoja wa Vijiji vya Nyuki Duniani, Umoja wa Vijiji vya Nyuki Tanzania. Dhana (Concept) ya Kijiji cha Nyuki ni kubwa na imepokelewa vizuri duniani. Na sisi hapa tuna-perfect hii idea na kwa maana hii itawezesha pia Serikali kutenga maeneo makubwa kwa ajili ya Vijiji vya Nyuki.
SWALI: Nchi yetu tunajua imebarikiwa ardhi kubwa, lakini bado tuna changamoto ya matumizi bora ya ardhi na ndiyo tunakuwa na migogoro katika maeneo mengi, changamoto hii unaitazama vipi katika muktadha wa kuwezesha uanzishaj wa Vijiji vya Nyuki?
JIBU: Mimi kwanza, naona tofauti na watu wengine wanavyofikiri. Mimi naona kwamba ardhi ni mali, ardhi ni asset kwa hiyo mtu anaweza kuamua atumie hela zake kununua ardhi au vinginevyo. Kwa hiyo mimi badala ya kwenda kununua bia nyingi za kunywa kila siku, nimeamua kununua ardhi. Mwekezaji ndiye anaamua awekeze kwenye nini.
Kwangu nasema kwamba hakuna uhaba wa ardhi kabisa katika nchi yetu, bali tuna uhaba wa mawazo jinsi ya kutumia ardhi. Mfano mimi ukiangalia eneo langu hili ndilo eneo baya kabisa katika maeneo haya kwa maana ya mawazo ya wakulima na wafugaji maana ni eneo lenye mawemawe ambalo mtu hawezi kulima. Kumbe watu walikuwa wanaangalia maeneo kwa mtazamo wa kilimo, mimi maeneo yote mabaya nataka niyanunue na nauziwa bei ndogo kwa sababu eneo kama hili la mawemawe utalima nini?
Kwa maana nyingine kwa sababu kazi yangu mimi siyo kulima, ni kwenda kuweka mzinga tu pale na kuhifadhi. Ndo maana hapa mnaweza kuona kama limeendelezwa sana, lakini mimi hapa siendelezi chochote mimi nimeacha miti inakua, inarefuka. Niseme tu ukiona mfugaji yeyote anagombana na mkulima ujue kwamba ni tofauti za fikra. Kwamba mfugaji anawaza kwamba yeye ndiye mkubwa na huyu mwingine anawaza kwamba yeye ndiye bora kuliko mwenzake, ubabe tu wa kawaida. Ubabe wa watu na siyo ubabe wa asili (nature).
Mimi naweza kusema kwamba serikali kupitia maliasili na utalii inatambua kwamba nyuki wanapaswa kufugwa kwenye eneo kubwa. Kwa hiyo nao wametenga hifadhi za serikali za nyuki ambazo ziko hapa Manyoni, ziko Handeni, zipo Kibondo, zipo maeneo mengi. Kuna maeneo ambayo miaka 40 iliyopita serikali kuu ilianzisha mashamba makubwa matano, na hivi karibuni Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania baada ya kuanzishwa mwaka 2013 pia wameendelea kuwaomba wananchi na serikali za mitaa waendelee kuwapa mapori ili wayatunze. Kwa mfano miaka miwili iliyopita walikuwa wameuomba msitu Minyughe ambao ulitengwa na Wilaya ya Singida (zamani) ambayo sasa ni Wilaya ya Ikungi, ni heka nyingi sana zaidi ya 200,000.
Na mimi nawaambia siku moja fanyeni utaratibu muwaita watu mia wakataji wa mkaa na watu mia warinaji wa asali, wakikaa kwenye chumba kimoja angalia tu hata afya zao…utaona hawa warina asali wana afya ya aina gani na hawa wakata mkaa watakuwa na afya gani, yaani tuanze tu na pale!.
Mimi niseme kwamba kwa ujumla mimi sioni kama kuna uhaba wa ardhi. Kwa sababu ardhi hata kama haina miti, tutaipanda. Tutachukua mbegu kutoka huku iliyopo na kuipanda. Mimi ninaona kuna tofauti ya fikra na naona kama watu wengi wanapenda sana asali, wanapenda sana mazao ya nyuki, lakini hawapendi establishment zake. Natoa tu ushauri kwamba watu wawapende nyuki kwa faida ya wao leo za vizazi vijavyo. Nyuki anahifadhi mazingira.
Mimi nashangaa Wizara ya Maliasili na Utalii wanatumia nguvu kubwa kujaribu kuhifadhi misitu, lakini ukiweka tu nyuki itahifadhika maana hakuna mfugaji nyuki ambaye hukata miti. Na mimi nawaambia siku moja fanyeni utaratibu muwaita watu mia wakataji wa mkaa na watu mia warinaji wa asali, wakikaa kwenye chumba kimoja angalia tu hata afya zao…utaona hawa warina asali wana afya ya aina gani na hawa wakata mkaa watakuwa na afya gani, yaani tuanze tu na pale!
Nimefurahi sasa hivi miongozo mingi ya serikali kwa mfano kwenye sera ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ni kweli kwamba mtu binafsi anaweza akamiliki hifadhi yake ya misitu.
Halafu tuje kwenye mawazo, mtu anayekata miti. Unakata miti unatengeneza mkaa unakwenda kuuza gunia, huo mti ungetundika mzinga mbona ungepata magunia mengi ya mkaa kwa miaka inayokuja? Kwa sababu thamani yake ni kubwa. Au badala ya kuchoma mkaa kwa nini tusingesema tuje tufanye sustainable harvesting tukate baadhi ya miti mikubwa, tutengeneze mizinga mingi tuweke (kwa ajili ya kufugia nyuki). Mimi naona hakuna kitu cha kufuata Ulaya hapa, ardhi ipo ya kutosha.
Nimefurahi sasa hivi miongozo mingi ya serikali kwa mfano kwenye sera ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ni kweli kwamba mtu binafsi anaweza akamiliki hifadhi yake ya misitu, unaimiliki vizuri kabisa hata kama ekari ngapi unamiliki. Lakini Mtanzania mmoja tu ndiye anayemiliki hifadhi Tanzania. Sasa nikachunguza nikaona ni nini, kwamba wale ambao wana-promote ile sera hawai-promote vizuri. Wange-promote wakaweza wazi kwamba ukitaka kumiliki hifadhi binasfi hii……kwa sababu unawaambia watu wafuge nyuki, sawa, lakini utafugia angani? Watafugia mahali mbako leo na kesho patatangazwa kwamba hapa pameishakuwa hifadhi?