27.2 C
Dar es Salaam
HomeMwelekeoProf. Mkenda: Kilimo kitatuvusha tukiongeza tija, ufanisi... (iv)

Prof. Mkenda: Kilimo kitatuvusha tukiongeza tija, ufanisi… (iv)

Anayepeleka ni bwana shamba na bwana shamba atajuaje kitu kilichotafitiwa miaka mitano iliyopita, na yeye miaka 25 iliyopita tangu atoke chuoni atakaa kijijini anakunywa wanzuki tu! Kwa hiyo lazina tuwafanyie mafunzo rejea. Ni kweli maofisa ugani ni wachache tuna uhaba mkubwa kupindukia, lakini hata waliopo lazima wafanye kazi vizuri. Sisi tulichoanza nacho tumesema hawa waliopo tuwatumie sawasawa, huku taratibu za kuwaajiri wengi zaidi zikifanyika.

SWALI:

Unafikiri kuna haja ya kujikita katika maeneo ya kipaumbele maalum kama matatu au manne ili tuweze kufanikiwa zaidi kuliko sasa tunapogusia kila kitu?

“Lakini tunajua nguvu za soko ndizo zitaamua.”

PROF. MKENDA: Tumekuwa tukishughulika na mazao karibu yote; chai, tumbaku, kahawa, pamba, korosho na mkonge. Tumerudi kujikita kwenye mkonge, tumeanza kujikita kwenye michikichi, tumeenda kwenye alizeti, tumeenda kwenye zabibu….sasa kwenye utafiti kwa kiasi fulani nilipenda wawe na uwanda wa mpana kuchgua kitu ambacho kinaamsha udadisi wao.

Ukiwa wanataka kufanya utafiti kuhusu dengu, wafanye, kuhusu beans wafanye, lakini haya maeneo mengi nayo tafiti ziendelee. Muhogo kwa mfano wafanye utafiti na wanatuonyesha kwamba matokeo yanaweza yakawa mazuri. Hili suala la kusema tuchague mazao, maana yake ni nini? Kama ni kampeni hiyo tumefanya. Lakini sasa kwa mfano kilimo cha ufuta kimeibuka na kinakwenda kwa kasi kubwa, hakuna mtu alichagua ila nguvu za soko. Ukienda kule Lindi hivi sasa kilimo cha ufuta kinakwenda vizuri kwa sababu wako wanunuzi.

Kama serikali ukisema sisi huku tungependa korosho, sidhani kama itakuwa sahihi. Nadhani kuna hiyo kampeni ambayo tunafanya kuimarisha mazao na tumechagua zabibu. Hapa karibuni tumejaribu kuzungumza, lakini tunajua nguvu za soko ndizo zitaamua. Hata parachichi siyo sisi tulianza, walianza wakulima, na hapo sasa sisi ndo tukang’amua ahaa mbogamboga…mazao ya bustani ngoja tuyawekee mkakati kuyaendeleza Pengine isingekuwa hivyo, sisi tungeendelea tu na mazao ya kawaida. Vitu vya aina hiyo vitaibuka na unaona soya inaaza tena kwa kishindo kwa sababu ya uhitaji wake.

Je, wakijua kwamba nikifanya hivi nitapata pesa wataacha kufanya? Kwa kweli kazi yetu ni kuongeza tija kwenye kilimo na masoko, ninaamini watalima.

SWALI:

Vijana wetu kwa kiasi kikubwa wavutiwi na kilimo. Wengi ambao wangeliweza kujihusisha na shughuli hii unawakuta wako mijini wakijisughukisha na uchuuzi ambao kwa kweli hauatwavuhsa. Nini kifanyike vijana wavutike kwenye kilimo?

 

PROF. MKENDA: Kuna vijana wameamua kujikita kwenye kilimp. Kwa mfano wapo waliojiunga na sasa wanalima pilipili kule Mvomero wakimaliza kuzalisha tunawasaidia. Hawa wametoka wanameanzisha mashamba yao wenyewe. Na wakipata pesa hawa vijana, maana wanachotafuta ni pesa watakaa, maana wanakikimbia kilimo kwa sababu wanaona hakuna pesa. Na siyo kwamba wanakataa kulima kabisa, hapana. Hawa vijana ukiwaona kazi wanayofanya barabrani kwenye jua ni ngumu sana. Hawakai kwenye kiyoyozi bali wanazunguka na vitu wanatembea. Je, wakijua kwamba nikifanya hivi nitapata pesa wataacha kufanya? Kwa kweli kazi yetu ni kuongeza tija kwenye kilimo na masoko, ninaamini watalima.

Kuna vijana huwa wanatolewa pale Sokoine wanapelekwa Israel na wanakwambia kilimo kule ni kiwanda, na watu wanafanya kazi muda wote hakuna muda wa kupoteza. Kila kitu kinaendeshwa kwa mitambo na kompyuta kwenye kulima. Wakirudi sasa tunaona wanakuja wanapotea wanaanza shughuli nyingine ni wachache sana wanarudi kwenye kilimo. Kwa  hiyo hapo Mvomero watakaokuja hapo ni hao baadhi ambao wametoka Israel. Kuna kampuni inaitwa NOSC (Njombe Out-growers Service Company) wale kinamama wanasema vijana hawataki kazi ya chai, lakini wenye pia wanasema kwa kuwa wanataka kwenda kuendesha bodaboda, tuleteeni hiyo mashine ambayo ni kama bodaboda, unaendesha shambani huku unavuna. Kwa hiyo vijana wakipata hiyo wataendesha huku wakivuna badala ya kwenda barabarani kusubiri abiria, na maisha yatakwenda mbele. Kwa kweli kazi ni kukifanya kilimo kiwe cha kuvutia zaidi.

Na vilevile kuna mitaji ya kuanzia, hii changamoto hiyo. Mfano wale vijana nilikuwa nao pale waliniambia wamepata eneo katika Halmashauri ya Lushoto, lakini changamoto ni mtaji.Hata kama kijana anataka kulima anasema mimi nataka kwenda kule Kiteto kuchukua shamba kubwa nilime mahindi ya njano na soko liko pale, lazima uwe na mtaji wa kuanzia. Ndo maana nimesema katika vipaumbele vyetu ni pamoja na hiyo agro-financing katika mambo tunayopaswa kufanya. Tumeunda na tutazindua timu ya kufanya utafiti vizuri kwenye agro financing na mambenki wamenikubalia kukaa katika hiyo kamati na nimemwambia Bashe (Hussein, Naibu Waziri wa Kilimo) ataiongoza itafanya kazi kama miezi mitano, lakini itakuwa na sekretariati yenye nguvu ambayo itakuwa ikikusanya taarifa. Kimoja ambacho nimekiona juzi nilipokuwa Morocco, ukiwekeza vijijini kwenye kilimo, riba ni asilimia moja au moja na pointi kidogo, wao kwenye kilimo riba inacheza zaidi ya asilimia mbili.

Sisi kwetu benki ya kilimo imejitahidi kufikia asilimia tisa ambayo bado ni kubwa sana kwenye kilimo. Japo kuna watu bado wanapata mkopo nimeona nimekwenda Mbarali kutoa matrekta makubwa, combined harvester ambalo mtu anakwambia hili litalipa nikilifanyia kazi. Sasa tunahitaji kupanua zaidi, of course mtaji uwepo na vijana waandaliwe. Pia fursa za kulima ambazo zina matokeo ziwepo. Akilima asipoweza kuuza hilo ni tatizo. Kama nilivyosema maeneo ambayo tuna supply constrains kwa mfano ukaamua kulima alizeti unapewa mkataba wako kabla ya kuingia shambani, unalima wakati unajua nani ananunua. Ni rahisi zaidi kuwa na mpango wa kifedha. Hata hivyo nisijibu kana kwamba ni jambo rahisi, ni pasua kichwa inabidi tukifanyie kazi sana.

SWALI:

Kuna changamoto ya mazao kupotea baada ya msimu wa mavuno (post harvesting), hili nalo tunalitazamaje?

 

PROF. MKENDA: Kwa kweli kupotea mazao baada ya kuvuna bado ni tatizo kubwa kwenye kilimo chetu. Tumeongeza uwezo wa kuhifadhi mazao. Kwenye nafaka sasa hivi tunaweza kuhifadhi hadi tani 500,000, kwenye hivyo vihenge tuna tani kama109,000 na tuna mradi mkubwa wa namna ya kutunza mazao hasa dhidi ya sumu kuvu ambao unafanyika hapa wizarani. Kingine ni logistics kwa ajili ya kuchakata mazao ya kilimo haraka. Hilo ni suala kubwa ambalo nalo tunalitilia maanani maana kweli upotevu ni kubwa hata ukizungumzia tija upande mmoja ni kama upotevu unakata hiyo tija upande mwingine.

SWALI:

Kuna shida ya ulaghai kwenye vyama vya ushirika, kuna malalamiko kwamba wakati mwingine wanapopeleka mazao hawapati kinachostahili. Mnalitazamaje suala hilo?

 

PROF. MKENDA: Kwanza dhana kuu ya vyama vya ushirika ni kwamba ni taasisi za wananchi wenyewe, na ushirika ni hiari yao na kwa kuanzia tu ni kwamba sisi serikali tunakuwa na mipaka. Tutajitahidi sana kuhakikisha kwamba hakuna anayedhani kwamba chama cha ushirika ni shirika la umma au taasisi inayopewa amri na Waziri wa Kilimo au mtu mwingine yeyote kwa kuingiliwa sana operesheni zao. Lakini wajibu wa serikali kwa sababu chama cha ushirika chochote ni taasisi ya umma japo siyo ya serikali, mtu akidokoa kwenye vyama vya ushirika hataachwa salama. Serikali imefanya kazi kuangalia udokozi na mikataba mibovu na mali nyingi sana imerudi kwa sababu ya ufuatiliaji wa serikali kwenye vyama vya ushirika. Jambo la pili tuna taasisi yak ukaguzi ni kama CAG inaitwa COASCO inakagua hesabu za vyama vya ushirika ripoti yake iliyotoka baada ya ukaguzi kufanywa. Sasa hivi hakuna chama cha ushirika hata moja imepata hati safi.

Serikali imefanya kazi kuangalia udokozi na mikataba mibovu na mali nyingi sana imerudi kwa sababu ya ufuatiliaji wa serikali kwenye vyama vya ushirika.

Nimewamibia Tume ya Ushirika waiweke ripoti ya ukaguzi kwenye website na wanachama waipate na waijadili. Kuna sehemu nyingine hupati hati safi kwa sababu hujaweka mtaalamu wa kuweka hesabu vizuri. Inawezekana hujaiba, lakini hesabu hazijawekwa vizuri. Lakini vilevile Shaban Robert alituambia mali bila daftari hupotea bila habari, sasa  kama huweki kumbukumbu vizuri tutajuaje kama inapotea na kama inapotea kwa ubadhirifu? Na sisi (serikali) tunasimamia kwa maana hiyo kuhakikisha kwamba ile mali ya wanachama inalindwa kwa manufaa ya wanachama na inazingatia maamuzi ya wanachama na siyo kikundi cha watu wachache.

SWALI:

Kulikuwapo na progamu mbili kubwa za kilimo; ASDP I na ASDP II, je tuna lolote la kujivunia kutokana na utekelezaji wa program hizi?

 

PROF. MKENDA: Kikubwa kwanza kwa mafanikio yetu katika kilimo kutokana na hizi programu ni kwamba tunajitosheleza kwa chakula sana na tuna ziada ya mchele, ziada ya mahindi, tuna chakula cha kutosha na ziada. Kwa hiyo tatizo sasa hivi limekuwa ni kutafuta masoko. Lakini bado tungependa kuongeza tija zaidi ili kuhimili ushindani katika hayo masoko tunakotaka kwenda kuuza. Kwa sababu unachukua mahindi unapeleka Lubumbashi ambako unapambana na mtu anatoka South Africa, ambaye tija yake ni kubwa zaidi. Japokuwa supply line ni ndefu, lakini anaweza kushindana na wewe sawasawa. Hata kwenye nafaka, nyingi tunaweza kulima kwa ajili ya mifugo, lakini lazima tija yetu iwe kubwa, tupate ugali wetu tule na tuwe na mahindi mengine ambayo yatazalishwa kwa ajili ya mifugo na itawezesha watu kuacha kuwa wachungaji na badala yake kuwa wafugaji.

Usambazaji wa pembejeo haujawa bila mikwamo kama ambavyo tungelipenda iwe, hata hivyo hii ni hatua tumepiga.

SWALI

Wewe ni Waziri wa Kilimo, ikiwa ungeondoka leo ni jambo gani ambalo ungependa ukumbukwe kwalo?

 

PROF. MKENDA: Bado ni mapema mno kusema ni legacy gani ningependa kuiacha, kimsingi natamani nisiondoke haraka kwa sababu yako mambo ambayo tumejipanga na ninatamani nione matokeo. Tuna kampeni ya alizeti ambayo tunaifanya kama crash program, mifumo ya kusambaza pembejeo na tuna changamoto kwenye korosho. Lakini kumbuka kuwa tulichokifanya mwaka huu ni tofauti maana baada ya mavuno mazuri ya 2017/18 ambao wakulima walipewa ruzuku ya asilima 100 ya pembejeo, ruzuku yote ikaondoka wakawa wanajitegemea wenyewe na uzalishaji ukashuka sana. Kwa hiyo mwaka huu tumeamua tutafute namna fulani ya kuhakikisha wanapata pembejeo. Sasa ule mfumo haujafanya kazi vizuri. Usambazaji wa pembejeo haujawa bila mikwamo kama ambavyo tungelipenda iwe, hata hivyo hii ni hatua tumepiga. Kwa kweli kuna muda kidogo kuja kujua nini kitakuwa na matokeo. Sasa ni kama miezi saba nadhani tu, karibia minane na kazi ndo inaanza.

spot_img

latest articles

explore more

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here