27.2 C
Dar es Salaam
HomeMahojiano‘Lazima tuache tabia ya kuwapuuza wakulima’

‘Lazima tuache tabia ya kuwapuuza wakulima’

Katika Makala haya waandishi wetu, Jesse Kwayu na Neville Meena, wanazumngumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), ….., ambaye anaeleza matamanio yao katika kuinua sekta ya kilimo nchini. Fuatana nasi katika mahojiano haya.

SWALI: Miongoni mwa mambo yanayotajwa na wakulima kuwa kikwazo katika shughuli za nao ni sheria na sera zinazoongoza sekta ya kilimo kwa upana wake. Nini nafasi ya MVIWATA katika kushughulikia changamoto za aina hii hasa ikizingatiwa kuwa mara nyingi sera na sheria hupendekezwa na serikali?

“Kuwasaidia wakulima wanachama waweze kuelewa kwamba ni sera gani imeibuka, sheria gani imeibuka na inaweza ikawa na mchango au athari gani kwa maisha ya mkulima.”

JIBU: Kama alivyosema mwenyekiti ni kwamba, kati ya kitu muhimu katika kujenga mazingira mazuri ya kilimo, kufanya kazi vizuri ni sera na sheria na kwa hiyo sisi tunachokifanya kama taasisi ni tunajaribu kufuatilia sera na sheria mpya kadri zinavyoandaliwa.

Lakini cha pili, ni kuzichambua na kuona yapi ambayo yana athari kwa wakulima wadogo  na kushauri nini kifanyaike kutokana na uchambuzi yakinifu ni kazi ambayo tumekuwa tukifanya mara kwa mara.

Lakini pia tumejaribu kushauri wale wanaotunga hizo sheria, na ipo mifano mingi ambayo tumeifanya, mchango ambao tumeutoa wakati ambao umepokelewa tumeboresha sana sera na sheria hizo. Kwa mfano sheria ya kilimo, hapo ilikuwa ni muswada ambao tuliupitia vizuri na maboresho tuliyoyafanya yamechukuliwa na muswada ule ukawepo sheria, lakini pia kuna mifano mingi tu ya sheria na sera na kanuni mbalimbali ambazo tumejaribu kuzichambua kwa pamoja, kwa hiyo huu ndo mchango.

Lakini pia ni kuwasaidia wakulima wanachama waweze kuelewa kwamba ni sera gani imeibuka, sheria gani imeibuka na inaweza ikawa na mchango au athari gani kwa maisha ya mkulima.

walau tunafahamu kwamba kuna azimio ambalo liliwekwa kwa nchi za Kiafrika za kuongeza bajeti za kilimo walau isipungue asilimia 10  la pato la kitaifa.

SWALI: Ni nini mtazamo wenu wa mabadiliko yoyote ambayo pengine serikali inakuwa inayafanya kwa maana ya bajeti inapotenga fedha kwa ajili ya shughuli za kilimo?

JIBU: Tunashukuru kila mara tunapopewa heshima hiyo ya kuhudhuria mawasilisho ya bajeti ya kilimo. Kama unavyofahamu sasa hivi bajeti ni nyenzo muhimu na kiashiria muhimu cha dhamira ya serikali kubadili au kuendeleza mfumo wa kilimo.

Kwa hiyo kwa sasa hivi kwa hali ilivyo, walau tunafahamu kwamba kuna azimio ambalo liliwekwa kwa nchi za Kiafrika za kuongeza bajeti za kilimo walau isipungue asilimia 10  la pato la kitaifa.

Kwa hiyo sasa ambacho tumekiona ni kwamba bajeti haijakua kufikia kiwango kile ambacho kinatokana na azimio la mataifa ya Kiafrika ya kufikia asilimia 10 ya bajeti ya taifa.

Sasa hivi unaweza ukaangalia kwa mfano bajeti ya kilimo ya mwaka huu ni bilioni 280 hadi 290 hivi, unaweza kuona ni asilimia ngapi ya bajeti yetu ya kitaifa na mwenendo huo umekua ndivyo ulivyo. Kwa hiyo inaweza ikaashiria kwamba dhamira ya kusukuma kilimo kulingana na mahitaji ya kirasilimali haijatosha.

SWALI: Tanzania tuna bahati ya kuzungukwa na nchi takriban nane hivi na karibu nchi zote zina mahitaji ya chakula, unafikiri ni kwa nini tunashindwa kutumia masoko yetu effectively yanayozunguka nchi? Lakini jambo la pili, unazungumziaje utaratibu wa serikali kuwazuia wakulima kuuza mazao yao katika masoko hayo ya nje?

JIBU: Nianze na hilo la mwisho ya dhana juu ya mkulima, na hasa niseme mkulima mdogo. Kuna dhana ambayo imejengwa sana kwamba mkulima anaonekana kama mtu asiyekua na uwezo wa kufikiri, asiyekuwa na uwezo wa kupanga, kuamua na kwa hiyo lazima kuwe na mtu mwingine wa kufikiri kwa niaba yake, wa kupanga kwa niaba yake na hata ikiwezekana wa kuongea kwa niaba yake.

Na ni mtazamo mbovu sana kwa bahati mbaya. Ni mtazamo ambao umechangia katika kudidimiza uwezo wa ukuaji wa wakulima na ndio maana umesema mwenyewe kwamba mkulima anaonekana kama mtoto.

Kwa hiyo wakati anapoamua yeye mwenyewe kuanza kulima kwa zao alilolichagua mwenyewe, hakuna anaesema chochote. Wakati wa kuvuna hapo ndipo watoa maamuzi wanaingia na kumpangia kwamba wewe utakufa na njaa, utakuja kututesa sisi na kutuombaomba chakula. Kwa hiyo hakuna kuuza. Sasa shida yake ya kwanza inaua ubunifu na ukiangalia wakulima sio kwamba sisi sijui nyinyi wenzangu, lakini mimi nimekulia katika familia ya wakulima na ndicho kilichonikuza mimi.

Kwa hiyo naelewa tangu nikikua wazazi wangu wakipanga kulima heka ngapi kichovunwa kitauzwa kiasi gani kitauzwa, kiasi gani kwa ajili ya mbegu kiasi gani na kwa ajili ya chakula. Kwa hiyo mpango wote huu ndio tuliokua nao.

Sasa mkulima anaweza akasema kwamba mahindi makavu haya hayatanilipa ngoja niuze mahindi mabichi, akitaka kutoa tu kakutana na amri marufuku katika wilaya yangu kuuza mahindi mabichi. Sasa afanyeje mkulima huyu? Ameshaona mahindi makavu hayamlipi na mahindi mabichi yatamlipa na ameshakutana na amri ambayo msingi wake haueleweki. Sasa atakuwaje mbunifu na atawekaje rasilimali zake afikie kinachoitwa tija, kwa hiyo hii ni eneo la kwanza.

Tuliwahi kuwatuma wanafunzi ambao walikuja kwenye mazoezi hapa kwetu (MVIWATA) wapite banda kwa banda katika maonyesho ya Mwalimu Nyerere na kimsingi ni kwamba cha kwanza tulichogundua siyo chini ya nusu ya bidhaa zinazoonyeshwa siyo za kilimo, bali bidhaa za kilimo ni sehemu ndogo.

SWALI: MVIWATA kama taasisi ya wakulima imekuwa mshiriki wa maonyesho ya kilimo ambayo hufanyika kanda mbalimbali kila mwaka, kwa mtazamo wako ni ipi tija ya maonyesho haya kwa wakulima hasa wadogo nchini?

JIBU: Sina tathimini halisi, lakini labda nirejeshe ile histori nzima, historia ni kwamba maonyesho ya nanenane ambayo awali yalikuwa yanafanyika sabasaba, yalikuwa na lengo la kuwawezesha wakulima kujifunza maarifa mapya kwenye kilimo. Watumie siku hiyo kuonyesha  na hata kutambua thamani ya kilimo na mchango wake na hata wakulima wenyewe kwa ustawi na maendeleo na uchumi wa taifa letu.

Sasa taratibu taratibu, ninaweza nikadhani kwamba kilihama, yaani maonyesho yalihama kidogo kutoka kujikita katika masuala ya kilimo zaidi yanaweza kuhamia kwenye maonyesho ya kibiashara zaidi. Tuliwahi kuwatuma wanafunzi ambao walikuja kwenye mazoezi hapa kwetu (MVIWATA) wapite banda kwa banda katika maonyesho ya Mwalimu Nyerere na kimsingi ni kwamba cha kwanza tulichogundua siyo chini ya nusu ya bidhaa zinazoonyeshwa siyo za kilimo, bali bidhaa za kilimo ni sehemu ndogo. Cha pili wanaoingia kuangalia maonyesho yenyewe asilimia ya wakulima ni wachache mno na wengi ni watu wa mjini ambao wanaenda kuangalia, na siyo kuangalia kilimo bali wanaenda kutafuta bidhaa mikanda, beseni ya plastiki na mengine mengine vinavyouzwa kwa bei nafuu kidogo.

tunafanya maonyesho ya nanenane hivi tumeshawahi kujiuliza yana thamani kwetu au tunafanya kwa sababu ni utamaduni.

Lakini pia wanaoonyesha wengi ni kutoka halmashauri kwa gharama fulani kwa sababu ukijumlisha pia na gharama za kuingia kwenye nanenane halafu umtoe mkulima ambae haishi mjini ametoka kijijini, asafiri, ikiwezekana asiweze kurudi siku hiyo, sidhani kama imepewa tija ya kutosha. Sasa ndiyo maana nakumbuka aliyekuwa Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba aliwahi kuongea na mimi nakumbuka vizuri ikiwa Arusha na akasema tunafanya maonyesho ya nanenane hivi tumeshawahi kujiuliza yana thamani kwetu au tunafanya kwa sababu ni utamaduni.

spot_img

latest articles

explore more

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here