31.7 C
Dar es Salaam
HomeUncategorizedMageuzi ya kilimo yatawezekana tu kwa umwagiliaji

Mageuzi ya kilimo yatawezekana tu kwa umwagiliaji

URUSI ilipoivamia Ukraine Februari 24 mwaka 2022 ghafla dunia nzima ilipata madhara makubwa ya upungufu wa nafaka ya ngano pamoja na bidhaa zake. Upungufu huo ulitokana na shehena ya ngano ambayo hulimwa kwa wingi Ukraine kushindwa kusafirishwa. Kwa maana hiyo dunia nzima ilipata upungufu wa bidhaa za jamii ya ngano kwa sababu tu mata[1]tizo yalitokea Ukraine.

Ukiitazama Ukraine yenye ukubwa wa kilometa za mraba 603,628 ikiwa na ardhi ifaayo kwa kilimo yenye ukubwa wa hekta milioni 41.3, ni ndogo kuliko eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye ukubwa wa kilometa za mraba 945,087 ikiwa na ardhi ifaayo kwa kilimo yenye ukubwa wa hekta 44.

Kwa ulinganifu huu unaweza kujihoji ni kwa nini Tanzania siyo mzalishaji mkubwa wa zao lolote duniani kiasi kwamba iwe ndiyo tegemeo kuu? Hali ya Tanzania kutokuwa na nguvu kubwa sana katika uzalishaji wa mazao ili iwe tegemeao kubwa la usalama wa chakula la dunia, inaweza kufungamanishwa na mfumo wetu wa kilimo cha kutegemea mvua.

Mazao mengi yanayolimwa nchini hapa kwa kiwango kikubwa yanategemea mvua. Kama mvua hazikunyesha, basi huo unakuwa ni mwaka wa hasara siyo kwa wakulima tu, bali pia kwa usalama wa chakula nchini.

Ni katika kutambua umuhimu wa kujiweka kwenye nafasi ya kuwa mzalishaji mkubwa wa mazao mbalimbali ya kilimo, kama mahindi, maharage, ufuta, alizeti, michikichi, pamba, kahawa na mazao mengine ya mbogamboga, serikali imeamua kuingia katika kazi kubwa ya kuleta mageuzi katika kilimo kwa kusukuma mbele ajenda ya kilimo cha umwagiliaji.

Miongoni ni mwa juhudi hizi ambazo tunasema zinastahili kuungwa mkono na kutengewa fedha za kutosha, ni mkakati wa kufufua skimu zote za umwagiliaji nchini, pia kujenga mpya ili kuongeza uwezo wa taifa kuendesha kilimo cha umwagiliaji.

Kilimo cha umwagiliaji kinatoa fursa kwa wakulima kufanya kazi ya uzalishaji mashambani mwaka mzima, tofauti na kilimo cha kutegemea mvua. Katika kufanikisha mkakati huo, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imeingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili kujenga mabwawa sita kwenye ukanda wa Reli ya Kati maeneo ambayo yamekuwa korofi kwa mafuriko.

Maeneo ambayo mabwawa haya yanakwenda kujengwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2024/25 ni pamoja na Dabalo, Buigiri, Hombolo, Kimangae, Kidete na Ikowa. Maeneo haya yanapatikana katika mikoa ya Mageuzi ya kilimo yatawezekana tu kwa umwagiliaji TAHARIRI Morogoro na Dodoma.

Kujengwa kwa mabwawa haya kutaongeza shughuli za kilimo cha uhakika na hivyo kuongeza thamani ya adhi ifaayo kwa kilimo nchini. Mbali na mabwawa haya, pia serikali inatekeleza miradi mingine ya umwagiliaji katika maeneo tofauti nchini ambako jumla ya miradi 780 yenye thamani ya Sh. bilioni 366.5 inatekelezwa.

Miradi hii ilianza kutekelezwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2022/23 na kazi inaendelea. Ingawa serikali imekusudia kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji hadi kufikia hekta milioni 1.2 ifikapo mwaka 2025, matarajio halisi ni kwamba hekta 983,466.06 sawa na asilimia 81.95 ya lengo zitapatikana ifikapo mwaka 2025.

Ni matamanio ya umma wa Watanzania kwamba kwa neema ya ardhi ifaayo kwa kilimo ambayo nchi hii imejaliwa sasa tutaanza kujiweka kwenye nafasi ya kuwa nchi tegemewa kwa uzalishaji wa chakula duniani. Hali hii siyo tu itatujengea heshima, bali itasaidia kujenga uchumi imara wa nchi na kwa mwananchi mmoja mmoja.

Kwa miaka na miaka nchi yetu imekuwa inasumbuliwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na kupata mvua nyingi, hata hivyo badala ya kutumia mvua hizo kujenga akiba kubwa ya kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, tumekuwa tulilalamika huku tukipoteza rasilimali hiyo adhimu kwa kujaza bahari.

Sisi tunaamini Ukraine imejiweka kwenye nafasi hiyo ya kuwa tegemeo kubwa la nafaka ya ngano duniani kwa sababu wamewekeza kwenye kilimo, wamejenga miundombinu ya kusaidia kilimo kuwa shughuli yenye tija kubwa. Ni kwa kufuata nyayo kama hizo tu ndipo nasi kama taifa tunaweza kunufaika na adhi kubwa ifaayo kwa kilimo ambayo Mola ametukirimu.

spot_img

latest articles

explore more

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here