SWALI: Vipi kuhusu ajira, Kijiji kimeajiri watu wa ngapi kwa ajili ya shughuli za hapa?
JIBU: Hapa nafanya kazi na watu ambao wako kwenye pay roll wako themanini. Wahitimu wa vyuo vikuu wako 39 na hao wengine ni vijana ambao kazi zao ni kutunza mizinga, na wengine wako kiwandani wanachakata (asali), wengine mmewaona wanasimamia ofisi hapa, ila naona kama nimechelewa. Wazo langu lilikuwa kwamba kufikia mwaka 2020 (mwaka jana) niwe nimeajiri watu 6,000. Lakini bado sijafanikiwa kwa sababu nilivyokuwa nimewaza kwenda ni tofauti na uhalisia.
“Kwa mfano, utalii wa nyuki. Watu wengi hawajui utalii wa nyuki na mimi sikuwaza.”
Na hapa nakubaliana na ile kauli inayosema mipango mara nyingine siyo matumizi. Na ni kweli mara nyingi na kwa watu wengi, mipango huwa siyo matumizi. Barcode inaweza ikazidi kwa uzuri au inaweza ikapungua, inategemea. Na mimi naona kuna vitu vingine ambavyo sikuviwaza kama vitatokea katika Kijiji cha Nyuki. Kwa mfano, utalii wa nyuki. Watu wengi hawajui utalii wa nyuki na mimi sikuwaza.
Utengenezaji wa mizinga, sikuuwaza mimi. Mimi nilijua nitatunua mizinga, lakini kwa sababu suppliers, yaani wale waliokuwa wananiletea mizinga walikuwa wananisumbua na mimi ndo nikaamua kuanza kutengeneza mizinga mwenyewe hapa,. Nikaanzisha karakana ili kuondoa huo usumbufu. Lakini kitu kingine ambacho sikukitarajia ni kwamba nimetengeneza lile bwawa ambalo nimezuia maji pale, lile bwawa niliwaza natengeza kwa ajili ya mimi na nyuki wangu. Lakini hivi karibuni mpaka watu wa dini (wakrito) wamekuja kuanza kubatizana humu. Wale watu wa ubatizo wa maji mengi.
nilimpoteza mtu ambaye nilikuwa nampenda sana. Mchumba wangu. Kwa sababu mimi tu ni mfuga nyuki.
Hivyo ni vitu ambavyo vingine sikuviwaza, lakini nikaja kujua kwamba kumbe kwa kuwepo Kijiji cha Nyuki kuna vitu vingi vinatokea. Utoaji wa mafunzo mimi sikuwaza. Ila sasa kwa sababu watu wengi hawajui nyuki na mimi naona kama nisiposambaza haya maarifa haya niliyonayo naona nitakuwa natenda dhambi. Hii ni dhamiri yangu naona kama nitaulizwa wewe ulikuwa unafahamu haya mambo na hukuwaambia watu. Nimeamua niwaambie watu na wasipofanya, na hizo dhambi zihamie kwao.
SWALI: Kuna jambo lolote ambalo unajutia katika kufanya kazi hii ya ufugaji wa nyuki?
JIBU: Ndiyo vipo; kwanza kabisa nilimpoteza mtu ambaye nilikuwa nampenda sana. Mchumba wangu. Kwa sababu mimi tu ni mfuga nyuki. Yeye hakutaka kwenda kunitambulisha nyumbani kwao kama mfuga nyuki na mimi nilimwambia kwamba mimi ni mfuga nyuki. Yeye alitaka akaremberembe kwamba hafugi kawaida ila anafuga kitaalamu, mimi nilimwambia kwamba sitaki uniite jina lolote zaidi ya mfuga nyuki. Alipokwenda nyumbani alipoulizwa kwamba mchumba wako anafanya kazi gani, alishindwa kusema ni mfugaji wa nyuki. Hilo ni jambo ambalo najutia.
Jambo jingine ni mimi kuitwa mchawi. Mtanzamo (Perception) ya watu kwa kushindwa kujua mimi nafanyaje, walianza kuniita freemason huko nyuma, kile nacho niliona kwamba mimi watu wananiona nini (japo mtu hutakiwi kufuata hayo ni kawaida), lakini mimi naona kwamba kwa nini hawa waniseme hivyo? Sawa ila jingine niseme kwamba kwa ujumla ni kwamba zamani mimi nilikuwa mjinga sana. Nilikuwa sijui jinsi haya mambo yalivyo na katika process labda kuna wateja wangu ambao sikuwahudumia vizuri. Kwa kutowa-treat vizuri na kipindi hicho wao walikuwa serious, sasa hivi naona kama wengine niliwapoteza kwenye biashara. Lakini
namshukuru Mungu kwamba sasa nimepata wateja wengine ambao kwa kutumia yale makosa ya kwanza, sasa nina watu ambao nawa-handle vizuri na mambo yanakwenda vizuri.
Kwahiyo ni vitu ambavyo (majuto ni kawaida) lakini kwa ujumla ukiacha hayo majuto, mimi nafurahi sana na sasa nina mpango wa kuanza kuwekeza kwenye starehe na raha. Kwa mfano hapa kijijini ninaweza kuwekeza kwa kuwanunulia watu muziki na watu kucheza kila Jumamosi. Kumbe nimegundua kwamba watu hawapati raha katika maisha yao, wakifikiri mpaka upate raha inabidi utumie nguvu kubwa sana. Watu hawajui kufanya vitu vya msingi sana, very basic. Kwa mfano watu wengi sana hawajui kulala. Hawajui. Kulala tu kwa standard za UN, hamna mtu anayejua namna nzuri ya kulala. Kuna watu wanaishi muda mfupi simply kwa sababu hawajui kulala. Yaani jinsi la kulala. Wengine wanala hivi (kifudifudi), wengine wanalala hivi (chali) yani tofauti tu.
Kumbe nimegundua kwamba watu hawapati raha katika maisha yao, wakifikiri mpaka upate raha inabidi utumie nguvu kubwa sana.
Lakini watu wengi pia hawajui kula. Vyakula viko vingi, lakini hawajui kula. Lakini kuna watu hawajui kuvaa. Analala vizuri, anakula vizuri lakini anavaa vibaya. Lakini kuna watu wanafanya vitu vingi vizuri, halafu wanafikiria vibaya. Yaani simple tu anafikiria vibaya, anajikuta kwenye matatizo. Kwa hiyo mimi nilikuwa nawashauri katika kipindi kijacho, nitaanzisha programu ya kuwafundisha watu darasani; raha ni nini, shida ni nini, kwa sababu watu hawajui tofauti kati ya shida na raha.
SWALI: Kijiji kimeanza na safari inaendelea, ukitazama mbele unaona nini hapa katika Kijiji cha Nyuki?
JIBU: Nikiangalia mbele katika mtazamo wa miaka mitano au kumi ijayo, naona Chuo Kikuu kimejengwa hapa kikiwa na ushirikiano na vyuo vingine duniani maarufu, kikiwa kinafanya tafiti na kutoa majawabu ya mambo makubwa sana. Watu wengi sana watasoma hapa. Lakini nikiangalia Kijiji cha Nyuki naona kama kuna hoteli kubwa kuliko hotel zote Singida. Na hoteli hii naona watu wanakuja kwenye hii hoteli simply kupumzika, lakini pia kula raha.
naona maisha mazuri; naona matibabu, naona watu wakiwa wanapata mawazo makubwa hapa na naona sisi pia tukiishi muda mrefu.
Naona wale wanaoondoka hapa wanaondoka na zawadi za mazao yote ya nyuki. Pia naona makumbusho ya nyuki. Naona watalii wengi wamesafiri kuja hapa kuona na kujifunza masuala ya nyuki. Naona watoto wa shule za msingi, sekondari na wanavyuo wakiwa wanakuja hapa kujifunza mambo haya ya nyuki kupitia makumbusho. Lakini naona maisha mazuri; naona matibabu, naona watu wakiwa wanapata mawazo makubwa hapa na naona sisi pia tukiishi muda mrefu.