*Kwa wengi mkulima ni kama tusi
SWALI: Sawa sheria ina changamoto, ulitaka vikundi hivi viendeshwe pasipokuwa na sheria au ni yapi mawazo yako katika suala hili?
Hakuna jambo ambalo unaweza kuliendesha bila vyombo vya sheria. Sheria ni kitu muhimu sana kwa sababu inawapa uwezo kuendesha vizuri kile chombo chenu.
Tunachosema kwamba mchakato mzima wa kuanzisha sheria hii, hawakushirikisha wale wanaoanzisha huu ushirika, wangewashirikisha wakulima huenda wangetoa mawazo yao ambayo yangeweza kusaidia kuwekwa kwa sheria ambayo ingekuwa rafiki na wale watu wanaohusika.
SWALI: Kitu gani kifanyike kwenye hiyo sheria ili iwe rafiki?
JIBU: Kwanza, leo ukizungumzia mtaji wa milioni 10 kwa baadhi ya vikundi ambavyo vina nia ya kuanzisha ushirika wao ni tete. Sasa hili la mtaji tete, mimi nadhani sheria ingeliangalia vizuri kwa sababu inaua yaani wale ambao walikuwa na nia ya kuanzisha ushirika.
“Kwa kweli tulikuwa tunawasiwasi tunaweza tukatafuta msomi ambaye tukaweza kumuajiri, akasema ukitaka kuua Saccos yenu basi mpeni msomi.”
Lakini, la pili ukiingalia kwa mfano ile sheria inataka wale watendaji angalau awe na mtaalamu, lakini sisi tuna uzoefu kuna Saccos ambazo mpaka sasa zinachechemea. Kwa mfano hii ya kwetu hatujapata sisi huyo mtaalamu ambaye amesomea masuala sijui ya nini hayo, ameendesha mkulima, lakini ukiangalia uendeshaji wake wamekuja wakaguzi wa COASCO taasisi ya serikali, mara mbili kukagua kile chama kwa kweli changamoto zake ni chache mno.
Nanukuu mmoja akasema: ‘Kwa kweli tulikuwa tunawasiwasi tunaweza tukatafuta msomi ambaye tukaweza kumuajiri, akasema ukitaka kuua Saccos yenu basi mpeni msomi.”
Kwa hiyo tunafikiria sisi kwamba wangetoa, sheria isingebana mtu mwenye uwezo hao watu wameanzisha ushirika wao na kuna watu wana uwezo, unajua uongozi unaweza usisome, lakini uongozi ni karama mtu anaweza akazaliwa na karama.
Kwa hiyo watu kama hao tunawatumiaje kwa sababu sheria inakuja inawabana, tunawatoa watu wenye karama kwa sababu ya kigezo tu cha sheria.
hata picha tu ukiangalia za kuhamasisha kilimo sidhani kama zinamhamasisha kijana aone kama ni fursa.
SWALI: Kilimo na vijana; kwa nini vijana wengi ambao ni nguvukazi ya taifa hawataki kujihusisha na kilimo na baala yake wanakimbilia mjini kufanya uchuuzi wa bidhaa za kutembeza mkononi?
JIBU: Kilimo ni sekta muhimu hususani katika nchi yetu, inaajiri watu wengi sote tunaamini hivyo, lakini ni sekta ambayo ndiyo inayosaidia uhai wa watu sababu bila kilimo sidhani kama tunaweza tukakaa hivi tukazungumza.
Tunaona nchi inapokabiliwa na upungufu wa chakula unaona athari, wakati mwingine serikali inatumia fedha nyingi kuagiza chakula kutoka nje kwa ajili ya kuja kusaidia wananchi wake.
Kwa hiyo tunapozungumzia kilimo, tunazungumzia jambo kubwa sana, changamoto ya vijana mimi nadhani ni mfumo tu, wakati mwingine unakuta mkulima anaitwa we mshamba, we mkulima.
Na hii dhana imetuingia hata sisi wakulima, tumekuwa hatuna hata ujasiri leo hii ukiulizwa unafanya kazi gani yaani mtu uzungumze kijasiri kabisa kwamba mimi ni mkulima. Yaani unaona kama vile kazi ya watu ambao hawajaenda shule, ndivyo inavyochukuliwa katika nchi hii.
Sasa vijana wana changamoto nyingi, kwanza naweza nikasema kwamba mfumo, yaani kinavyochukuliwa kile kilimo na jinsi kinavyopigiwa chapuo, hata picha tu ukiangalia za kuhamasisha kilimo sidhani kama zinamhamasisha kijana aone kama ni fursa.
Kwa sababu unamkuta kazee kamevaa nguo zimechanika chanika na kajembe ka mkono, hizi sidhani kama ni picha ambazo zinaweza zikamfanya mtu apende kilimo.
Lakini cha pili, mimi natoka Kiteto na naweza nikasema katika maeneo au katika wilaya ndani ya nchi hii ambazo unaweza kuwa na wilaya ambayo ina eneo kubwa na watu wanatumia maeneo makubwa kwa shughuli za kilimo kama Kiteto. Kiteto mtu kulima heka 200 au 300 ni jambo la kawaida, na wengine wamekwenda mbali zaidi wamelima mpaka eneo laki moja.
Shamba unatembea kwa mguu unaweza ukatembea kutwa nzima. Hiyo ndo hali ya Kiteto. Sasa hawa wanaomiliki haya mashamba wamejikuta watu wanamiliki maeneo makubwa makubwa, vijana hawana mashamba.
SWALI: Kwa hiyo katika muktadha huo unadhani nchi yetu ina tatizo la ardhi?
JIBU: Tatizo la ardhi nchi hii hakuna kwa sababu ukiangalia kuna maeneo mengi, ukichukulie Kiteto, tunazo hifadhi nyingi mno, ukubwa wa eneo la Kiteto lina kilometa za mraba 16,800 na kitu, lakini ni eneo ambalo linatumika katika shughuli za kilimo ufugaji na makazi ni kilometa za mraba kama 3,800 kama na kitu. Hizo nyingine zote ni hifadhi ambazo zimeanzishwa.
Huko shuleni na kwenyewe hawafunsishi kilimo. Kilimo ni kama adhabu. Ikikosa unapea kazi ya kulima. Nani atakipenda kilimo ambacho kimeheuza kuwa adhabu?.
Pamoja na hili linalofaa kwa shughuli za kilimo, waliojitwalia maeneo makubwa makubwa ni watu waliokuwa na hela zao. Wengi wanakodi mashamba, kwa hiyo hii ni changamoto pia kwa vijana wengine wanaona bora nikahangaikie mjini.
Lakini changamoto ya pili, kilimo kina changamoto ya masoko, kwa mfano haya mazao tunayozalisha, sasa ni kijana gani ambaye ataingia shambani azalishe mahindi yake ayauze Sh. 40,000 kwa gunia la kilo mia na akiuza anakata mtaji wake. Hiyo nayo ni changamoto kwa hiyo tunapoteza nguvu kazi ya vijana wanaacha kuzalisha wanakwenda kufanya kazi za kuuza njugu, wanauza maji, lakini tunaacha kwenye shughuli ambayo kwa kweli ingeweza kuwasaidia. Huko shuleni na kwenyewe hawafunsishi kilimo. Kilimo ni kama adhabu. Ikikosa unapea kazi ya kulima. Nani atakipenda kilimo ambacho kimeheuza kuwa adhabu?
SWALI: Je, vyuo havina mchango wowote katika kilimo?
JIBU: Wapo wasomi ambao kwa kweli wanaguswa na maisha ya wakulima na wanaguswa na sekta hii ya kilimo. Si wote inawezekana akawa yuko chuo kikuu, lakini sasa wanaotengeneza mifumo ya sera na nini, kwa hiyo unakuta kwamba lazima jitihada zao wakati mwingine zinapwaya.
Wako wasomi, na sisi tunao, hata hapa taasisi yetu watendaji wetu ni wasomi, wapo ambao kweli kwa maslahi ya wakulima wadogo, lakini wapo ambao kwa kweli wapo kuwaona kwamba wakulima wadogo kama ni washamba, yaani wapo tayari kusimama kwamba kwa hili haliwezekani, wakaweka misimamo yao. Kwa hiyo wasomi wapo, lakini sio wengi.
ni kijana gani ambaye ataingia shambani azalishe mahindi yake ayauze Sh. 40,000 kwa gunia la kilo mia na akiuza anakata mtaji wake.
SWALI: Tunafanyaje ili tuone kwamba kilimo ni mali ya wote na kila mmoja akitukuze na kukiona kama sehemu ya maisha yake?
JIBU: Watu kama nyinyi ,watu wa habari ni muhimu sana, mnao mchango mkubwa wa kuweza kuhabarisha umma kutoa huo mtazamo uliopo wa kuona kilimo ni kama adhabu, ni kazi ambayo haina maana. Kwa hiyo kwa kushirikiana na sisi kama wakulima na mashirika yanayofanya kazi na wakulima, mimi naamini mwisho wa siku watu wataelewa mchango uliopo katika sekta ya kilimo.