27.2 C
Dar es Salaam
HomeKilimo BiasharaParachichi: Dhahabu ya kijani wilayani Rungwe (ii)

Parachichi: Dhahabu ya kijani wilayani Rungwe (ii)

KUHUSU AJIRA

Kilimo cha parachichi kinatoa fursa nyingi za ajira kuanzia uandaaji wa mashamba, upandaji, palizi, utunzaji na hata uvunaji.

Rodgers Mwasambili ni mkulima wa zao la parachichi katika kijiji cha Ma, naye anaeleza kwamba vijana ya watatu walipata ajira katika shamba lake lenye ukubwa wa ekari mbili.

“Kila hatua ina fursa ya ajira mfano unavyoandaa shamba watu lazima wafyeke, wachimbe mashimo, lakini pia tunatumia mbolea ya samadi hivyo lazima uajiri vijana wa kubeba samadi kutoka kwenye makazi ya watu hadi barabarani.

“ili mkulima apate matunda bora ni vyema akatumia mbegu bora ambazo zimeandaliwa kitaalam.”

“Wanapakia kwenye gari na kuimwaga shambani, hiyo pia ni ajira, lakini kuna upandaji wa miti na kufunika majani shambani,” anasema Mwasambili.

Mwambungu pia anaeleza kwamba ameajiri vijana wanne wanaomsaidia katika shughuli mbalimbali za shambani.

WATAALAM WANASHAURI NINI

Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Rungwe, Juma Mzara, anasema parachichi ni tunda la kibiashara.

Anasema ili mkulima apate matunda bora ni vyema akatumia mbegu bora ambazo zimeandaliwa kitaalam. Anaeleza kwamba mbegu hizo zinatakiwa kukaa katika kitalu kwa muda kati ya miezi sita hadi tisa ndipo zipandikizwe shambani.

“Wakulima wengi wameingia katika uandaaji wa mbegu holela, wanajipandikizia tu kienyeji na madhara yake wanakosa faida kwakuwa hawawatumii maofisa ugani katika shughuli hiyo, hivyo kujikuta wakiambulia hasara badala ya faida,” anasema Mzara.

Anasema wakulima wanapotumia mbegu ambazo hazijaandaliwa kitaalamu, kuna uwezekano mkubwa wa kupata matunda yasiyokuwa na ubora pamoja na miti kushambuliwa na magonjwa mbalimbali ya mimea.

Kwa upande wake Neema Mwaigaga ambaye ni mtaalamu wa kilimo cha parachichi katika kiwanda cha Kuza Afrika ambacho kinasindika maparachini, anaeleza kwamba ili mkulima wa zao hilo  apate  faida ni lazima apende kilimo toka moyoni kabla ya kuwekeza.

Mwaiganga anasema hali hiyo itamsaidia mkulima kuzingatia kanuni zote za kilimo hicho badala ya kuingia kutokana na tamaa ya mafanikio ya watu wengine.

Anasema ili mkulima apate parachichi bora ni vyema akawekeza zaidi kwenye utunzaji wa shamba lake kwa kuzingatia elimu inayotolewa na maofisa ugani kwenye kilimo hicho.

kwa sasa wananunua maparachichi yote kwa ajili ya kukamua mafuta.

Mwaiganga anabainisha kuwa ili kupata maparachichi yenye viwango stahili, Kampuni inawajibika yenyewe kuvuna matunda shambani kwa mkulima kwa kuzingatia kanuni za uvunaji wa tunda la parachichi tayari kwa ajili ya kulipeleka sokoni.

Kuhusu changamoto ya wakulima kurejeshewa matunda yao kutokana na kutokidhi ubora (reject) na kukosa soko la kuuzia parachichi hizo, Ayida Munyali ambaye ni Meneja wa Kiwanda cha parachichi cha Kuza Afrika anasema kwa sasa wananunua maparachichi yote kwa ajili ya kukamua mafuta.

“Sisi kama kampuni ya Kuza kwa sasa tuna kiwanda kwa ajili ya kukamua mafuta hapa nchini,  hivyo baada ya kuvuna tunachambua ili kutenganisha first class (daraja la kwanza) kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi na yanayobakia yote tunakamua mafuta hapa hapa nchini,” anasema Munyali.

UANDAAJI WA MASHAMBA

Mzara ameeleza kwamba njia bora ya uandaaji wa shamba la parachichi ni kuzingatia ukubwa wa shimo la kupanda lenye kina cha sentimita 60 na upana wa sentimita 60. Inashauriwa kitaalamu mkulima achimbe mashimo miezi mitatu kabla ya kupanda miche.

“Kwa hiyo hilo ni shimo la kiwango cha chini, mkulima ana uwezo wa kutengeneza shimo kubwa zaidi ya hilo kutokana na wingi wa mbolea aliyonayo kwani mara nyingi tunashauri watumie mbolea ya samadi, hivyo yaweza kuwa mita saba kwa saba au nane kwa nane kati ya mche na mche,” anaongeza Mzara.

“Mara nyingi parachichi za HASI inakaa muda wa miaka mitatu tangu kutoa kitaluni na kupandikiza shambani, kuanza kutoa matunda japokuwa inaweza ikatoa maua hata miezi mitatu baada ya kupanda maua hayo tunashauri yaondolewe maana hayana manufaa kwa mmea,” aliongeza Mzara.

Mzara ameongeza kuwa parachichi huwa linavunwa kwa awamu mbili kwa mwaka, ambapo mavuno yenye faida kubwa kwa mkulima ni baada ya miaka mitano hadi sita.

Kuhusu soko la parachichi anasema kutokana na barafu iliyomwagika kwa wingi nchini Brazil, itakuwa ni fursa kwa wakulima wengi mwaka huu nchini Tanzania wilaya ya Rungwe ikiwemo kupata soko la mazao yao.

Vijana wanachukua hela katika makampuni ili wakusanye parachichi kwa wakulima wanachokifanya ni kununua kwa bei pungufu.

Aidha kuhusu changamoto zilizopo katika soko la parachichi wilayani Rungwe, Mzara anasema halmashauri imeweka mkakati wa kuwaondoa watu wa kati (madalali) katika zao la parachichi  kwa kutumia mfumo wa vyama vya ushirika.

“Vijana wanachukua hela katika makampuni ili wakusanye parachichi kwa wakulima wanachokifanya ni kununua kwa bei pungufu ya shilingi 1,200 kwa kilo, badala ya 1,500 kwa kilo moja ambayo ni sawa na parachichi tatu au nne,” alisema Mzara.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka ofisi ya kilimo wilaya ya Rungwe kwa mwaka 2019/2020 jumla ya wakulima wa parachichi ni 4,431 waliozalisha parachichi na kuziuza kwa wanunuzi ambao ni makampuni mawili kutokea ndani ya wilaya na wengine 10 kutoka nje ya wilaya.

sasa Tanzania watauza matunda nchini humo kama wakulima wa nchi hiyo wanavyouza apple hapa nchini.

Akiwa wilayani Rungwe, Agosti 1, 2021, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema mgogoro wa kibiashara uliokuwepo baina ya Tanzania na Afrika Kusini kuhusu uuzaji wa baadhi ya bidhaa umeshughulikiwa na serikali, na kwamba sasa Tanzania watauza matunda nchini humo kama wakulima wa nchi hiyo wanavyouza apple hapa nchini.

Pamoja na hayo alitoa rai kwa wananchi wilayani Rungwe kuwarithisha watoto wao mashamba ya parachichi wangali wadogo ili waweze kufanikiwa kupitia kilimo hicho.

“Napenda niwaambie jambo hili Wana-Rungwe, kuweni na utaratibu wa kuwapandia watoto wenu miche ya parachichi wakiwa wadogo ili hata wakisoma wakirudi kutoka masomoni wasitegemee tena ajira bali watumie ile elimu waliyonayo kuendeleza kilimo cha parachichi,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

spot_img

latest articles

explore more

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here