31.7 C
Dar es Salaam
HomeKilimo BiasharaParachichi: Dhahabu ya kijani wilayani Rungwe (i)

Parachichi: Dhahabu ya kijani wilayani Rungwe (i)

Sabina Martin, Mbeya

INGAWA zao la parachichi linaonekana kuwa ni dhahabu ya kijani wilayani Rungwe mkoani Mbeya huku wakulima wengi  wakichangamikia fursa hii mpya ya kibiashara, kukosekana kwa elimu ya kutosha kwa wakulima wadogo juu ya utunzaji wa zao hilo kumeathiri ubora na kiwango cha mavuko.

Ukosefu wa elimu hiyo inatajwa kuwa ni changamoto zilizokwaza utunzaji wa miche kabla ya kupandwa, hali inayosababisha miti ya zao hilo kushambuliwa na magonjwa hivyo kushindwa kutoa matunda yanayokidhi ubora katika soko la ndani na nje ya nchi.

“Wastani wa miche 60 kati ya 100 sawa na asilimia 60 inaweza kukauka au kuoza.”

Wastani wa miche 60 kati ya 100 sawa na asilimia 60 inaweza kukauka au kuoza ikiwa shambani kama mkulima hatazingatia kanuni za kilimo, hali inayosababisha hasara kwa mkulima. Kwa wastani mche mmoja huuzwa kati ya Shilingi 3,000 na 3,500.

Kwa mujibu wa jarida la Ackyshine Kilimo, parachichi ni tunda linalostawi sehemu za baridi na maeneo ya Rungwe mkoani Mbeya na mkoani Njombe linastawi vizuri na huwa na afya nzuri.

“Linahitaji joto la wastani wa nyuzi joto 15-25, mwinuko wa mita 1,200 hadi 1,800 kutoka usawa wa bahari na udongo ambao unastawisha zaidi tunda hili unatakiwa uwe kichanga tifutifu usiotuamisha maji,” inasomeka sehemu ya Makala mojawapo katika jarida hilo.

ukianza kulima ni zao lenye changamoto kubwa za uendeshaji, ni zao linalohitaji muda mwingi pamoja na gharama pia tofauti na mazao mengine.

Kilio cha baadhi ya wakulima wilayani Rungwe ni kukosekana kwa elimu ya kutosha ya namna ya kulima kilimo cha parachichi chenye tija.

Mmoja wa wakulima wa parachini, Anania Simon Fungo, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mabonde, Kata ya Msasani wilayani Rungwe mkoani Mbeya anaeleza kwamba aliingia katika kilimo kutokana na kutamani mafanikio ya baadhi ya wakulima wenzake, lakini hajanufaika nacho kutokana na kukosa elimu juu ya zao hilo.

“Ukiwa nje ya zao la parachichi kila mtu anazungumzia uzuri wake, lakini ukianza kulima ni zao lenye changamoto kubwa za uendeshaji, ni zao linalohitaji muda mwingi pamoja na gharama pia tofauti na mazao mengine,” anasema Fungo.

“Nilinunua miche 100, baada ya kupanda miche 60 ilikauka na mingine kuoza. Nilipata hasara maana mche mmoja nilikua nilinunua kwa shilingi elfu tatu hivyo nikapata hasara ya Shilingi 180,000 hiyo ni kwenye miche tu. Bado mbolea na waliochimba mashimo ni gharama nyingine,” anongeza Fungo.

WANUFAIKA WA KILIMO

Parachichi kama matunda mengine, ukilima kitaalamu na ukaweka juhudi na maarifa ni zao linaloweza kumkomboa muhusika katika umasikini.

Gerald Mwasomola ambaye ni mkulima kutoka katika kijiji cha Mabonde kata ya Msasani wilayani Rungwe, ana uzoefu tofauti ambao ni chanya na anaeleza namna alivyonufaika kupitia kilimo cha parachichi.

Mwasomola anaeleza kuwa ili kupata faida katika zao la parachichi ni vyema kuwekeza zaidi na kuzingatia kanuni zote za kilimo. Anaongeza kuwa yeye aliwashirikisha wataalamu wa kilimo kuanzia uandaaji wa shamba, upandaji na hata utunzaji na kwamba sasa anafurahia mavuno kwa mwaka wa tano.

“Nilikuwa na matamanio kama ilivyo kwa watu wengine, lakini sikutaka kuingia kwenye kilimo moja kwa moja bali niliwatafuta maofisa kilimo wakanishauri kabla ya kuanza kulima,” anasema Mwasomola.

alilazimika kupanua shamba lake kutokana na faida aliyoipata kupitia kilimo hicho na sasa ana miche zaidi ya mia sita.

“Kilimo hiki ili upate faida ni lazima uwekeze zaidi kama ilivyo katika biashara nyingine, kilimo kinahitaji pesa na muda kwa ajili ya kutembelea shamba lako kutunza kama tunavyotunza watoto wetu,” aliongeza Mwasomola.

Naye Essay Mwambungu ni mwanamke mwenye umri wa miaka 68 mkazi wa Kata ya Kiwira na ni mmoja wa wakulima walionufaika kupitia kilimo cha parachichi.

Mwambungu anasema walianza kilimo akiwa na mume wake na wakati huo walianza na miche mia mbili, lakini sasa alilazimika kupanua shamba lake kutokana na faida aliyoipata kupitia kilimo hicho na sasa ana miche zaidi ya mia sita.

Tulifanikiwa kupata faida japokuwa haikuwa kubwa kwakuwa ilikuwa msimu wa kwanza, faida kubwa ilikuwa kuanzia msimu wa tatu wa mavuno.

Mwaka 2019 Mwambungu alifanikiwa kupata zaidi ya millioni 18 kutokana na zao la parachichi kutokana na mavuno ya mwaka mmoja kutoka katika miche 800 aliyokuwa nayo.

“Baada ya kustaafu tuliamua mimi na marehemu mume wangu kuanzisha kilimo cha parachichi, tulianza na miche 200 na tuliwasumbua sana wataalamu kuhusu elimu ya usimamizi wa shamba letu.

“Tulifanikiwa kupata faida japokuwa haikuwa kubwa kwakuwa ilikuwa msimu wa kwanza, faida kubwa ilikuwa kuanzia msimu wa tatu wa mavuno ikatufanya kuongeza shamba jingine,” alieleza Mwambungu na kuongeza:

“Baada ya kuipata ile milioni 18 nilitaka ninunue gari la kutembelea, lakini baadaye nikapata wazo la kujenga nyumba mpya na ya kisasa. Nikaanza kujenga natarajia mwaka huu nikamilise kila kitu kwenye nyumba yangu hii mpya ndipo nihamie.”

spot_img

latest articles

explore more

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here