31.7 C
Dar es Salaam
HomeKilimo BiasharaBashe aanza na mbolea

Bashe aanza na mbolea

Na Neville Meena

NI dhahiri kwamba Waziri Kilimo, Hussein Mohamed Bashe ameanza kutumikia nafasi yake mpya kwa kushughulikia suala la mbolea nchini. Lakini kwa upande mwingine ni mwendelezo wa kile alichokuwa amekivalia njuga wakati akiwa Naibu Waziri katika wizara hiyo hiyo ya Kilimo.

Bashe anakuwa Waziri wa Kilimo akichukua nafasi ya mtangulizi wake (aliyekuwa bosi wake), Profesa Adolf Mkenda ambaye amehamishiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan Januari 8, 2022.

“There are no secrets to success. It is the result of preparation, hard work, and learning from failure.”

Siku tano tu tangu alipokula kiapo cha kuongoza Wizara ya Kilimo (Januari 15, 2022), Bashe alimpokea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa katika kiwanda cha kuzalisha mbolea, alionyesha kuwa wamejiopanga kuhakikisha kuwa mbolea inapewa kipaumbele cha juu katika wizara hiyo.

Majaliwa alikwenda kukagua ujenzi wa Kiwanda cha Kampuni ya Intro Fertilizer cha Dodoma. Katika tukio hilo, ndipo Bashe alipoweka nadhiri ya kuhakikisha kuwa tatizo la mbolea linapungua nchini kama siyo kumalizika kabisa.

Great things in business are never done by one person. They’re done by a team of people.

Katika maelezo yake kwa Waziri Mkuu, Bashe aliweka bayana kuwa Wizara ya Kilimo itatoa ushirikiano wa kutosha kwa mwekezaji ili kukidhi mahitaji ya mbolea nchini ambayo alisema kwa sasa ni wastani wa tani 700,000 kwa mwaka, huku serikali ikitumia dola milioni 450 (karibu Sh. trilioni 1.04) kuagiza mbolea kutoka nje.

Kwa nini mbolea kwanza?

Pengine Bashe ameamua kuanza na mbolea kwani ni moja ya mambo ambayo yalionekana kuwaumiza vichwa yeye binafsi wakati akiwa Naibu Waziri, pamoja na aliyekuwa bosi wake Profesa Mkenda kuanzia katikati ya mwaka jana 2021.

Wakati huo, ndipo mbolea ilipoanza kuadimika, siyo Tanzania tu bali katika sehemu mbalimbali duniani huku takwimu za Benki ya Dunia zikiainisha kuwapo kwa ongezeko la bei ya bidhaa hiyo kwa mwaka 2021 ikilinganishwa na 2020.

Taarifa ya Benki ya Dunia iliweka bayana kwamba hali hiyo ilichangiwa na na changamoto ya upatikanaji wa malighafi kutokana na vikwazo vya kibiashara vikiweamo vinavyohusianishwa na UVIKO-19 pamoja na ongezeko la mahitaji ya mbolea duniani kwa asilimia 37.

Matukio hayo pamoja na mengine yalitajwa kuchangia ongezeko la bei ya mbolea nchini Tanzania kwa kiwango cha kati ya asilimia 20 hadi 38 kulingana na aina ya mbolea ndani ya mwezi mmoja kati ya Juni na Julai 2021.

Uchambuzi uliofanywa na Jukwaa la Wadau wa Kilimo Tanzania (ANSAF) kuhusu Hali ya Sekta Ndogo ya Mbolea ambao taarifa yake ilitolewa Agosti 4, 2021 ulibainisha kuwa ongezeko la bei ya mbolea lilitarajiwa kuongeza gharama za uzalishaji wa kilimo katika msimu wa 2021/2022, ikilinganishwa na msimu uliotangulia wa 2020/21.

Hali hiyo ni dhahiri ilisababisha kilio kutoka sehemu mbalimbali nchini ambako wakulima walipaza sauti wakilalamikia kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za mbolea, huku wakikabiliwa na changamoto ya soko la mazao yao kwa ajili ya kurejesha gharama za usalishaji na kupata faida kwa ajili ya kugharamia mahitaji yao mengine ya kimaisha.

Matumizi ya mbolea nchini

Akizungumza katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara mwaka jana 2012, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dk Stephan Ngailo, alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema matumizi ya mbolea nchini yako chini kulingana na vigezo vya azimio la Abuja la mwaka 2016.

Mkutano wa wakuu wa nchi uliofanyika Abuja mwaka 2016 uliazimia masuala mbalimbali katika kilimo ikiwamo kuongeza matumizi ya mbolea katika eneo la ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufikia angalau kilo 50 za viinilishe vya mmea (Plant Nutrients) kwa hekta.

Hata hivyo Dk. Ngailo anasema matumizi ya viinilishe vya mbolea kwa Tanzania ni kilo 19 kwa hekta ambayo ni sawa na asilimia 38 ya kiasi kilichopendekezwa katika Azimio la Abuja.

Anasema matumizi hayo madogo yanatokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na bei kubwa za mbolea kwa wakulima, masharti ya ulipaji yasiyozingatia mizunguko ya msimu wa kilimo, uelewa mdogo juu ya matumizi ya mbolea na wakulima kutokuwa na uhakika wa masoko ya mazao na hivyo kutoona tija ya kuwekeza fedha zao kwenye mbolea.

Kutokana na hali hiyo, Dk Ngailo anasema Serikali iliona umuhimu wa kubuni mikakati mbalimbali ambayo ingesaidia kuhakikisha kuwa bei ya mbolea inashuka na wakulima wanawekewa masharti rafiki ya kuilipia.

Taarifa ya Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 (Matokeo Muhimu Agosti 2021) inabainisha kuwa matumizi ya mbolea katika mwaka wa kilimo 2019/20 yalikuwa jumla ya hekta milioni 2.8 sawa na asilimia 20.1 ya eneo lililopandwa na kati ya hizo, hekta milioni 2.7 ni za Tanzania Bara na hekta 40,020 ni Tanzania Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mbolea za asili zimekuwa zikitumika zaidi ikilinganishwa na mbolea za viwandani na kwamba matumizi hayo yanatoa fursa ya kutafuta masoko maalum ambayo yana utayari wa kulipia bei kubwa kwa mazao yaliyozalishwa kwa mbolea za asili. Kitakwimu katika mwaka wa kilimo 2019/20, asilimia 60.6 ya eneo lililopandwa kwa kutumia mbolea za asili na asilimia 39.4 mbolea za viwandani.

I love those who can smile in trouble, who can gather strength from distress, and grow brave by reflection. ‘Tis the business of little minds to shrink, but they whose heart is firm, and whose conscience approves their conduct, will pursue their principles unto death.

Ahadi ya Rais

Katika hotuba yake ya kufunga mwaka jana na kuukaribisha mwaka mpya aliyoitoa Desemba 31, 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alizungumzia uhaba wa mbolea akiahidi kwamba serikali yake itachukua hatua za muda wa kati na zile za muda mrefu ili kuwaondolea adha wakulima.

“Tunatambua changamoto ya upungufu wa mbolea ambayo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na kushuka bidhaa hiyo duniani kwa sababu ya Uviko-19. Lakini habari njema ni kwamba mapema mwakani 2022 tunatarajia kupata mbolea ya kukuzia mazao itayouzwa kwa bei ambayo wakulima wameizoea,” alisema Rais Samia.

Katika hatua za muda mrefu, Rais Samia alisema serikali inaratibu ujenzi wa viwanda viwili vya mbolea ambavyo ni kile kinachojengwa mkoani Dodoma na Kampuni ya Intro Fertilizer na kingine ni kile kinachokusudiwa kujengwa mkoani Mtwara na Kampuni ya Dangote.

Kauli ya Rais kuhusu ujenzi wa viwanda hivyo ni kama mwitikio wa mapendekezo ambayo yamekuwa yakitolewa mara kadhaa na watalamu na wadau mbalimbali wa Kilimo kama moja ya hatua za muda mrefu za kukabiliana na uhaba wa mbolea nchini.

Miongoni mwao wadau hao ni Jukwaa la Wadau wa Kilimo Tanzania (ANSAF) ambao katika taarifa ya uchambuzi wake kuhusu mbolea, walipendekeza kwamba Serikali ichukue hatua za kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vya mbolea vya ndani na kuimarisha vilivyopo ili kuongeza uzalishaji na upatikanaji mbolea nchini.

Pendekezo hilo pia limo katika taarifa ya Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 (Matokeo Muhimu Agosti 2021) ambayo ilibainisha kuwapo kwa matumizi madogo ya mbolea katika uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini.

“Licha ya kuhimizwa kwa matumizi ya mbolea, bado mwitikio wa matumizi ni mdogo. Hali hii inaweza kuwa inachangiwa na bei kubwa za mbolea ya viwandani ambayo huagizwa kutoka nje ya nchi,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo na kuongeza:

“Sera zilenge kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vya kuzalisha mbolea nchini ili kupunguza bei zake na hivyo kuvutia wakulima wengi kuzitumia.”

Katika hotuba ya bajeti yake ya mwaka wa fedha 2021/22, Wizara ya Kilimo ilibainisha kwamba kwa mahitaji ya mbolea yalikuwa ni tani 718,051 kwa msimu wa kilimo uliotangulia wa 2020/2021.

Kwa mujibu wa hotuba hiyo, hadi Aprili 2021, upatikanaji wa mbolea ulikuwa umefikia tani 678,017 sawa na asilimia 94.4 na kati ya kiasi hicho tani 426,572 zilikuwa zimeingizwa kutoka nje ya nchi, tani 32,239 zikiwa zimezalishwa nchini na tani 219,206 zikiwa ni bakaa ya msimu wa 2019/2020.

The first rule of any technology used in a business is that automation applied to an efficient operation will magnify the efficiency. The second is that automation applied to an inefficient operation will magnify the inefficiency.

Bashe na mbolea

Bashe alianza harakati za kufuatilia mbolea tangu akiwa Naibu Waziri wa Kilimo kwani itakumbukwa kuwa Aprili 2021 aliiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) na wafanyabiashara wa mbolea nchini kuangalia uwezekano wa kuingiza mbolea ya mahitaji ya mwaka mzima kwa mara moja kupitia mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja, ili kuhakikisha pembejeo hiyo inamfikia mkulima kwa bei nafuu.

Katika harakati za kuhakikisha mbolea inapatikana kwa bei nafuu, Bashe alikwenda mbali zaidi akifuatilia mifumo ya usafirishaji wa mbolea kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam kwenda mikoa mingine akitaka utumike usafiri wa reli badala ya barabara.

Kwa mujibu wa Bashe mwaka 2021 gharama za kusafirisha mfuko wa mbolea kutoka Dar es Salaam hadi Tabora kwa barabara zilikuwa Shilingi 5,500 wakati kwa njia ya reli zilikuwa Shillingi 1,000/= tu sawa na tofauti ya asilimia sabini.

Katika kikao chake na waigizaji wa mbolea kujadili namna ya kutatua changamoto za waangizaji hao kilichofanyika Dar es Salaam, Julai 15, 2021 Bashe alisema: “Tutafanya kila jitihada ya kusaidia gharama zile ambazo zinaanzia kwenye bandari ya Dar es salaam kwenda kwa mkulima Kalambo kuzipunguza.”

Alisema tayari serikali ilikuwa katika mazungumzo na Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kuwezesha mbolea kusafirishwa kwa njia ya reli lengo kikiwa ni kupunguza gharama kwa mkulima.

Katika mazingira ya sasa ni dhahiri Waziri Bashe ana wajibu mbele yake wa kuchukua hatua madhubuti kuongeza uzalishaji wa mbolea nchini ili kuwawezesha wakulima kupata mbolea bora kwa wakati na kwa bei nafuu, hatua ambayo pia itaokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumika kuagiza mbolea nje.

spot_img

latest articles

explore more

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here